LOML | Love Of My Life (106)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:106
Kama mama naumia sana na tabia ya binti yangu ambayo anakuonesha, lakini nisikilize nimejaribu, nimepambana, nimemuomba sana msamaha.

Ni ngumu kukiri tena kwa kijana, mume wa binti yangu lakini nitafanya hivyo kwasababu mimi ni mtu wa kwanza natamani ndoa hii iendelee kuwepo leo na hata kesho.

Mwanangu, sijui hata utaniona vipi, naomba nisamehe lakini mimi ndiyo sababu ya binti yangu kuwa namna alivyo, na kufanya hicho anachosema lakini kiuhalisia huyu sio mwanangu mimi, sio mwanangu niliye mzaa mimi. Huyu sio yeye kabisa.

Mwanangu ni mpole sana, ni muoga sana, msikivu sana, mcheshi, mwenye upendo sana, na zaidi ya yote binti yangu ana huruma. Nilicho taka kwenye maisha yake ni kumfanya yeye binti mfalme tu.

Kuhakikisha anapata kΔ±la kitu.Hakosi chochote kile. Ni hadithi ngumu mwanangu, Ila kwakuwa naokoa ndoa ya mwanangu nitakwambia, nitasema kΔ±la kitu.

Mimi ni sababu ya yeye kuwa hivi alivyo, kitu natamani mzazi mwingine asiwe kama ambavyo nilikuwa mimi. Nikiwa bado msichana, wakati huo nimeolewa na yeye akiwa bado ni mdogo sana, msichana mdogo mno umri miaka minne mitano, alikuwa bado mdogo.

Baba yake alikuwa mtu wa safari sana, hata kuna muda nilimuhitaji sana lakini hakuwa anajali kuhusu mimi. Hata wakati akiwepo na bado mimi haoni mama ni mwanamke mzuri, haoni kuwa na mimi namuhitaji yeye sana.

Alichofanya yeye siku zote ni kuwaza mambo yake na maisha yake na nikithubutu kuhoji kwa upendo naambulia maneno ya shombo na kipigo. Kwa bahati mbaya sana haya yote mwanangu hakuwa anaya ona.

Alikuwa mdogo, siwezi mwambia na Mara nyingi yalitokea usiku sana. Lakini alikuwa anajua sina furaha hili Nina hakika kwasababu Mara nyingi alikuta nikiwa nalia sana.

Upo wakati mume wangu aliniita maneno mabaya sana, alinisema hata kuhusu mwili wangu akisema fuko wewe, jitazame ulivyo shepu ya simba, wewe ni mjinga sana, Nani atakutaka mwanamke huna akili kabisa, wewe ni mshenzi kabisa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata