LOML | Love Of My Life (110)

๐‹๐Ž๐Œ๐‹ (๐‘ณ๐’๐’—๐’† ๐’๐’‡ ๐’Ž๐’š ๐’๐’Š๐’‡๐’†) โฃ๏ธ:110
Mwanangu alilia kwa uchungu sana, nilipiga magoti pale nje nikisema โ€œNakupenda mwanangu, nakupenda sana kฤฑla sฤฑku. Kฤฑla kitu nafanya kwaajili yako wewe. Nataka uishi kwa furaha, nahangaika kwaajili yako wewe. Nipo tayari kufanya kฤฑla kitu kwaajili yako. Nimebadilika mimi kwaajili yako na unajua mama.โ€

Alilia sana, alilia kwa uchungu akisema โ€œumeniharibia maisha mama, ni wewe na sasa sioni thamani yangu kabisa.Unajua nini mama?, mwanaume wako, Jimmy alichofanya kwako, alifanya na kwangu Mara nyingi sana, alinipa chocolate, zawadi mbalimbali na alinifundisha kila kitu, amenifanya niwe hivi nilivyo, niwe mdhaifu na siwezi mama, siwezi kujizuia, Jimmy mama, ni Jimmy.โ€

Nilichoka, namfahamu Jimmy anaye zungumza naye hata mimi ndiyo alinichanganya kabisa akili kwenye mapenzi. Anapenda sana na anajua kutafanya lakini iweje alale na mwanangu bado mdogo na ni mtoto wangu inakuaje hana heshima hivi.

Nilichoka kabisa, hata kuinuka nilishindwa. Sikuweza kwa muda lakini mwanangu alikimbia kuelekea kwenye gari akilia. Niliona waalimu wakija nisaidia mpaka kwa gari.

Sikuweza hata kuendesha, nilimchukua mwanangu tuliingia kwa gari na mimi kutafuta msaada wa kufuatwa pale shule.

Nikiwa na mwanangu nililia sana nikiomba msamaha, nilisema kwa kulia โ€œnisamehe mwanangu, nakupenda sana, nisamehe sana binti yangu. Najua nimechelewa lakini nakuahidi nitashughulikia hili na utakuwa sawa mwanangu nakuahidi tafadhali nisamehe mama yako, sikuwa najua itakuwa hivi, sikuwa najua maisha yangu yatakugharimu namna hii. Nisamehe sana.โ€

Binti yangu alikuwa analia tu, natamani sana wakina mama wawe makini na watu wanaokuwa nao karibu haswa wakina mama wenye watoto. Watoto hawa wana waamini watu hawa kwasababu anajua tayari mama ana muamini hivyo ni mtu mzuri na mwisho wa siku wanafanyiwa mambo ya ajabu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata