
LOML | Love Of My Life (115)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:115
Niliinamisha kichwa changu huku nakikukuna na kilikuwa hata hakiwashi, baba yangu alikuwa anapiga pia, nilitazama simu na kupokea. Baba alisema βmwanangu Rodricky, Nilidhani unanielewa kijana wangu.β
Nilishusha pumzi na kusema βbaba kwasasa sipo tayari, sitamani kumuona.β
Baba alisikitika na kusema βmaisha sio rahisi hivyo kijana wangu haswa kwenye ndoa. Sitaki kuzungumza sana kwasasa, kwasababu hata mama yake ana tia huruma sana.
Baba yake pia hili linamuumiza sana. Imebidi tu waseme watakaa na mtoto wao. Hii inatupa ΓΌgΓΌmΓΌ sana sisi familia yako na tunaonekana Kama tunaungana na wewe. Kijana wangu, nakuomba sana usiwe hivyo.β
Nilishusha pumzi yangu kwa nguvu, na kusema βbaba!!β
Baba yangu aliniambia βsijui kuna kitu gani zaidi ya ulichoniambia. Lakini kusema ukweli mwanangu, mwenzio anajutia sana muda wote analia sana.β
Nilisema βbaba!!β
Baba aliniambia βmimi na mama yako tunarudi nyumbani. Tutawasiliana wakati ujao.β
Niliita Tena βbaba!!β
Baba yangu alikata tu simu.
Kwa mazingira haya, hata kazi ilikuwa ngumu sana kwangu. Nilikuwa nawaza mengi haswa kuhusu mambo mama yake mke wangu ameniambia. Mama mkwe wangu alikuwa anaumia sana, alikuwa analia sana.
Nilijisikia vibaya sana, lakini kama hivi ndivyo mbona mimi nampenda tu kwanini asitulie. Maskini dunia hii Ina mambo mengi sana ya maumivu. Maisha haya ni magumu sana. Watu wanapitia mambo mengi sana, watu wana trauma ambazo wanazificha na zinawaua kila siku.
Nilijikuta machozi yananitoka sana, malezi ya watoto ni muhimu sana. Kama mtu ameanza mapenzi umri mdogo namna hiyo. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kumfahamu mtu unayemuoa au kukuoa.