
LOML | Love Of My Life (116)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:116
Najua watu ni wazuri sana kuficha hadithi zao chafu, watu wengi sana kwenye vitabu vyao wanapenda kuachana kurasa mbaya na kubaki na zile nzuri tu kitu ambacho sio kizuri kwasababu ukweli ndiyo kitu pekee umuweke mtu kwenye maisha yake.
Mfahamu mtu unaenda kufunga naye ndoa, hata kama kwa kidogo tu. Na kamwe usipuuze ishara yoyote ile mbaya kwenye mahusiano yako. Zingatia ishara hizo. Zifanyie na uanze kuzifuatilia.
Zina maana kwenye maisha yako, upendo usikupumbaze, usiingie kwenye ndoa kwasababu tu unataka kuoa.Zaidi ni Mungu tu ndiyo anajua.
Huko awali nilisema βhakuna kitu kinatokea kwenye maisha yako kama bahati mbaya. KΔ±la kitu kimetokea kwasababu kilikuwa lazima kitokee.β
Nilikuwa naumia na mengi sana hapa, nilikuwa najisikia vibaya ndani ya moyo wangu. Nilikuwa nakumbuka nyakati tukiwa na furaha, namna alivyo mwanamke huku. Lakini nikikumbuka namna nimeumia nalia sana, naumia sana.
Kwenye haya maisha yako ya kΔ±la sΔ±ku, unaweza kumsamahe mtu yeyote Yule aliyekukukosea. Haijalishi kosa gani, haijalishi kamwe usisahau namna amekufanya ujisikie ndani ya moyo wako.Namna unajisikia ndiyo namna hiyohiyo itakufanya uweke mipaka kati yako na huyo mtu. Msamahe lakini usiache kusahau namna unajisikia.β
Nilikuwa nimekaa tu hapa nawaza hili na lile, lile na hili. Ilinichukua muda mrefu sana. Lakini ningefanya nini sasa zaidi ya kuendelea kutafakari maisha yanavyo nipeleka.
Ujumbe uliingia kwa simu yangu. Nilishika simu na kufungua ujumbe ule, alikuwa ni Gabriella na Aliandika βMume wangu, nisamehe tafadhali ππ, nitakufa bila wewe mume wangu, nitakufa mpenzi. Nitawezaje kuishi bila wewe.
Uwepo wako kwenye maisha yangu unanivusha na mengi sana. Kukosekana kwako kunasababisha shimo kubwa na refu sana ndani ya moyo wanguπ, mimi ni mjinga sana, nimepoteza, nimeharibu maisha yangu kwa kumpoteza mwanaume mzuri sana.
Mume wangu ninakuomba tafadhali, najua sina zuri La kufanya unikumbuke. Niamini mapenzi yangu kwako ni kweli kabisa. NISAMEHEπππ, bedoβ£οΈ nakuomba tafadhali, nimekosea, NISAMEHE ππππ.β
NAAAAM HUU NDIOOO MWISHO WA SEASON TWO