
LOML | Love Of My Life (118)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:118
Nilimtazama na kusema “na Hilo ndiyo tatizo lingine kaka. Mke wangu huwezi kudhani lakini ananitesa na kuniumiza sana. Sijui hata nikuambie nini, lakini Mke wangu ana mahusiano mengi mbali yangu mimi, tena sio na mwanaume mmoja. Inaniuma.”
Willy alinitazama na kusema “kivipi yaani, kabla yako au sasa hivi?”
Nilimuuliza Willy “unashangaaa nini?, kabla yangu ningelalamika nini kaka. Nimejaribu kuzungumza na mama yake naona tu ananipa hadithi nyingi hata sielewi.”
Willy alısema “miezi mitatu ya ndoa si ndiyo?”
Nilishusha pumzi, na Kisha Willy aliendelea kwa kusema “tukae rafiki yangu.”
Tulikaa na Kisha aliniambia “nitazame rafiki yangu.”
Nilimtazama na Kisha Willy aliniambia “rafiki yangu, kaka yangu, ndugu yangu. Siwezi kukushauri tofauti na ushauri was awali. Kitu pekee unaweza kufanya kwasasa ni kukaa na mke wako, kuzungumza kwa kına kujua tatizo ni jambo Gani.
Ninavyojua mimi, ndoa ni watu wawili wadhaifu, walio ungana na kuishi pamoja ili kukamilisha udhaifu wao. Watu hawa hawana budi kusaidiana, kuvushana kwenye magumu Yao, kuoneana huruma, kuombeana na kutunzana.
Ndoa yenu bado changa sana, miezi mitatu ndugu yangu, miezi mitatu hii mlitakiwa kuwa na furaha sana. Tafadhali ongeeni na wazee, msikilizane na mambo yaende sawa kabisa.
Nielewe kaka.Pengine mambo yatakuwa mazuri sana na hutoamini. Na Kama yakiwa mabaya zaidi başı nitakuwa sina budi kukuunga mkono kwa maamuzi yoyote Yale. Lakini kwanza tuokoe hii ndoa.”
Nililia nikisema “kaka nilifanya hivyo, nilimpa kila kitu, nikafanya kıla kitu sasa kwanini mimi simridhishi. Au nina kasoro kaka, eenh niambie Labda wenzangu kuna namna mnafanya wake zenu watulie mbona huyu wangu hanielewi?”
Kaka huyu aliniambia “wewe ni mwanaume mzuri sana, mwanaume ambaye kila mwanamke anataka kuwa naye. Kuna muda tu shetani anajiinua sana, kuna muda shetani hapendi ndoa zenye amani na furaha.

