
LOML | Love Of My Life (119)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:119
Kaka nisikilize, ukiwa karibu na Mungu wewe na familia yako na yeye atakuwa karibu nanyi. Trust me ninachokueleza No prayer goes in Vain(Hakuna maombi huenda bure) kila ukiomba Mungu anafanya namna. Nakuomba Kaka.โ
Nilimtazama tu, na wakati huo simu yangu ilikuwa inaita. Nilipo tazama alikuwa ni baba yangu. Nilishusha pumzi, na kusema โbaba tena.โ
Willy aliniambia โpokea kaka pengine kuna tatizo.โ
Nilipokea simu ya baba yangu, nilipoitq tu โbaba!!โ
Baba yangu aliniuliza โupo wapi?โ
Nilimwambia kwa upole โnipo na rafiki yangu baba, kuna tatizo?โ
Baba aliniambia โTatizo lipo, mkeo ametaka kujiua huko kwao, na unatafutwa hupatikani hivi kijana wangu una shida gani?โ
Nilishtuka na kusema โbaba unasemaje?, kujiua kivipi, una maana gani?โ
Baba yangu aliniambia โalikunywa vidonge vingi kwa wakati mmoja, muda huu ninavyo zungumza tupo hospitali. Fanya haraka Njoo hapa.โ
Nilichoka, hata kutoa machozi mimi nilichoka. Nilipokata simu nilisema โGabriella alitaka kujiua wapo hospitali.โ
Kaka Willy alishangaa na kusema โMungu wangu balaa gani hili, anaendeleaje?โ
Nilimtazama kaka Willy nikisema โsijui hata nilikosa wapi, baba anasema wanaendelea vizuri Ila wapo hospitali.โ
Willy alinitazama na kusema โtuondoke, fanya tuondoke.โ
Safari hii hata kubisha sikuweza, niliingia ndani ya gari na kuondoka na safari ilikuwa ni kwenda hospitali. Nilipofika pale mama yake Gabriella aliponiona tu alilia kwa uchungu akisema โalitaka kufa mwanangu, alitaka kujiua. Tafadhali yamalizeni mwanangu nakuomba.โ
Nilimtazama baba, na baba yake Gabriella walikuwa wamechoka wananitazama tu. Nilimkumbatia huyu mama ajisikie vizuri. Baada ya hapo niliuliza โmke wangu yupo wapi?โ
Mama alisema โamepewa dawa ili apumzike. Sidhani kama unaweza kumuona.โ

