
LOML | Love Of My Life (12)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:12
Tunapanga vitu huku yeye na simu, akimaliza anaweka pembeni kidogo inaita mpaka nachukia sasa niliamua nijikaze kama alivyosema wapo kwenye matatizo. Dereva alipiga simu kuwa amefika, nilimuelekeza afuate mizigo na kisha tuendelee na safari. Unajua tangu tunaingia ndani ya gari, mpaka tunafika nyumbani mke wangu na simu tu. Sikupenda kabisa hii tabia. Lakini nitafanyaje na nimeambiwa tayari kuwa ana matatizo.
Nilishuka na mke wangu, kama ambavyo ipo nyumba ni mpya lakini kila kitu kipo vizuri kabisa. Madam ambaye tumeandaliwa pale nyumbani alitupokea. Niliingia ndani na mke wangu.
Hakuoga hata zaidi alibadilisha nguo tu, alinibusu huku anaongea na simu na kuondoka zake. Nilibaki nina mshangaa tu mke wangu.
Nilipokuwa chumbani nilipata wazo nimpigie simu mama yangu, nilimpigia mama, mama alipokea na alisema βhutajwi mwanangu, tumetoka kuzunguma kuhusu wewe sio muda hapa, eenh niambie safari muda gani?β
Nilitabasamu na kisha nilimwambia βndiyo maana nimepiga nikujulishe kuwa hatujasafiri kuna changamoto kidogo.β
Mama alishangaa na kuuliza βnini tena?β
Nilielezea kwa udogo tu na mama alisema βooh jamani, Mungu awasaidie sana, naimani litapita tu.β
Nilisema kwa upole βhata mimi naamini hivyo mama, basi mimi napumzika kidogo tutawasiliana wakati mwingine, msalimie baba.β
Mama aliniambia βamekaa hapa anakusikia, amekukumbuka tu.β
Nikacheka na kusema βnawapenda wote.β
Tukacheka.
Nilijilaza kitandani, ile nafumba tu macho yangu. Yule binti huyu hapa, ninamuona kila mahali, naona kabisa amechukua moyo wangu, akili yangu, mawazo ana miliki mpaka usingizi wangu.
Nilifumbua macho na kusema βNi nini hiki, kwanini nakuwa hivi?β
Kabla sijajijibu simu yangu iliita. Niliitazama kwa muda na kutabasamu, alikuwa ni rafiki yangu. Nilipokea simu hii na kusema βkaka!!β