LOML | Love Of My Life (121)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:121
Nikiwa nimekumbatiana na Giana kwa uchungu sana. Nilimuachia na kuanza safari ya kutoka nje bila kujali mtu yeyote. Nilitoka, nilitoka na hata rafiki yangu alinikimbilia nilimwambia “nisamehe rafiki yangu, naomba Niache mwenyewe kwasasa. Nataka kuwa peke yangu tafadhali.”

Aliniambia kwa upole “Muda umeenda sana sasa, ni saa 2 na haupo vizuri Naomba nikuendeshe.”
Nilimtazama na kusema “Asante sana, nashukuru sana.Lakini nakuomba Niache tafadhali.”

Willy alinitazama tu na nikamwambia “No prayer goes in Vain. Nataka kuongea na Mungu peke yake sasa hivi, yeye ndiyo atanipa majibu ya matatizo yangu yote. Nimechoka sana.”

Sikutaka hata jibu lake niliingia ndani ya gari na kuondoka zangu, naelekea wapi, mimi sasa nilikuwa naelekea kanisani roho yangu ilikuwa inaniambia niingie kanisani nikakae tu hapo. Niliendesha gari kwa Muda kidogo na nilifika.

Baada ya kufika nilishuka, na wakati huo nashuka naona Pina ndiyo anaondoka. Nilijikuta namkimbilia. Nilipo mkaribia niliita “Pina!!!!”
Alisimama na kuitikia kwa kutaja jina langu “Rodricky!!”

Nilishusha pumzi, na Kisha Pina alisema “Uwe na jioni njema Rodricky.”
Nilimwambia kwa upole “tafadhali naweza kuzungumza na wewe?”
Pina aliniambia kwa upole “nilikuambia ukae mbali na mimi, nilikuambia hivyo ina maana hukumbuki?”

Nilivuta pumzi na kusema “wewe peke yako ndiyo unanielewa Pina. Nakuomba.”
Pina aliniambia “nipo na bibi yangu, nitamchelewesha.”

Nilimtazama na kusema “bibi namchukilia pikipiki, Kisha wewe nitakupeleka nakuomba.”
Pina alisimama akinitazama na najua wazi haoni alisema “haiwezekani.”

Alishikana mikono na bibi yake, nilijikuta kwa uchungu nasema “Pina amekunywa sumu, alitaka kujiua Kwasababu sijaweza kumsamehe.”

Halafu Nilishindwa kujizuia kuumia kabisa. Pina alisimama, Kisha niliona ananizungumza na bibi yake, halafu bibi alianza kuondoka na yeye alipiga hatua kunifuata. Nilisogea pia na kusema “Nimechoka Pina!!, Nimechoka sana.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata