
LOML | Love Of My Life (122)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:122
Pina alinikumbatia na kusema βPole sana Rodricky lakini leo sitakuwa na maneno mengi ya kukuambia na wala sitakuambia maneno laini ili tu unielewe.β
Nilimtazama na kusema βniambie chochote nijisikie amani nakuomba,β
Alinifuta machozi kwa mkono wake mmoja na kusema βnitakuambia haya kwasababu ndiyo njia pekee utanielewa Rodricky. Unatakiwa kujua kuwa sio kila mtu kwenye maisha yako anapokosea anatakiwa kupata nafasi nyingine ya kuendelea kukukosea kwasababu kiuhalisia ni kuwa watu wanapokosea wanajua kuwa wanakosea Ila wameamua kuchagua kukosea.
Mara nyingi watu wanakuona una maana kama tu una faida yoyote kwao.Na unapokuwa kwenye nyakati ngumu kama hΔ±zΔ± Hakuna mtu wa kukusaidia, kujisaidia ni jukumu lako wewe mwenyewe sasa uchague kuzama au kuwa mshindi.
Hakuna mtu wa kukuvusha mpaka ufungue moyo wako wewe mwenyewe kwasababu muda hauponyi kila kitu badala yake unaficha tu maumivu yako lakini baadaye utayakumbuka tena na Utalia ikibidi ili uwe sawa.
Kikawaida watu wanakutendea kulingana na unavyo Vumilia, ukivumilia leo kesho anaongeza anajua una uwezo wa kuvumilia.
Maisha yetu haya sisi wote tunavaa vinyago, ni vile tu wengine tunavaa vizuri tusionekane upande wa pili na wengine wanavaa vinyago sio vyao ndiyo wanaonekana wabaya mbele za watu haina maana wengine hawana upande wa pili.
Hata kama upo na kila kitu, kama huna ujasiri utadharaulika tu.Wema Bila mipaka, hukaribisha dharau kubwa sana. Ukiendekeza wema utakuwa unakosea kila siku kwasababu watakuumiza tu.
Hata siku moja mapenzi hayabadilishi mtu Bali maumivu, maumivu ndiyo hufanya tujue uwezo wa mtu kitabia.Kamwe huwezi mfurahisha mtu ambaye kwake furaha ina tafsiri tofauti hata yeye mwenyewe hajifurahii.
Wapi watu wanaomba msamaha ili tu waendelee kukuumiza ndiyo wanapenda hivyo.Amani ni gharama sana, Ina chukua akili, moyo, watu wako, na sadaka ya vingi kupatikana.
Gereza pekee gΓΌmΓΌ kulikimbia ni maumivu, maumivu, sio kila Vita ni za kupigana, zingine ni kuweka mipaka tu inatosha. Utahangaika sana Ila mtu anaweza tafuta mbadala wako kwa sekunde tu.