LOML | Love Of My Life (124)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:124
Nilishangaa kuona mama yangu, mama mkwe, wazeee watatu, baba yangu na baba wa mke wangu, padri, sister na mke wangu. Niliwakaribisha huku tayari nikijua nini kinaendelea.

Ninakumbuka sana pale sebuleni.Wazazi waliongea kuhusu upendo wao na wanatamani na sisi watoto tufuate.

Nakumbuka mama yangu alivyokuwa anasema β€œmwanangu, ndoa sio lele mama, nakuomba mwanangu msamehe mkeo, anakupenda sana sisi wote tumeona. Futa yote muanze upya ninyi bado vijana.”

Nilimtazama tu, baba yake Gabriella kwa Mara ya kwanza alisema β€œsisi binadamu tunakosea. Bahati nzuri wazazi wetu tupo hai na tunatamani Muwe pamoja mkiwa na lolote tuambieni kuliko kuvunja ndoa hii. Naomba sana wanangu, sipo tayari mnaachana.”

Padri alisema kwa kututazama β€œMungu anataka wana ndoa Muwe na furaha. Ukisoma Mithali 5:18. Ndoa ni muunganiko was kudumu vijana wangu. Mungu aliweka ndoa kwa kusudi maalumu, ndoa ni Mungu mwenyewe.

Anachukia sana kuachana na kugombana na sio rahisi kuvunja ndoa yenu.Ndiyo maana mna kula KIAPO cha kupendana maisha yenu yote. Ni kweli kuna kukosana, na ndiyo maana pia kuna upatanishi.

Wanangu, sio vizuri kugombana. Ni vizuri kuweka mambo yenu sawa na kuanza upya maisha mkishindwa kuna wazazi na sisi tupo yote haya ili Muwe na amani na furaha.

Wote wawili mna wajibu wa kutendeana kwa upendo na heshima na kushikamana kama familia. Kwasababu ninawafahamu muda mrefu sina maneno mengi ya kuwaambia nipo hapa nawaombea sana na nawaomba wanangu msikubali shetani aharibu hii ndoa yenu nzuri.

Kampeni ya shetani ni kuua ndoa zote na kitu kibaya ni tunaingia kwa kampeni hiyo bila sisi wenyewe kujua. Inaumiza sana.”

Wakati anasema hivyo mke wangu alianza kulia, wote tulimtazama, alipiga magoti katikati na kulia kwa uchungu akinifuata hata kunishika miguu yangu na kuilowesha machozi akisema β€œNipo tayari kuacha kila kitu lakini sio kukupoteza wewe mume wangu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BINTI MDUNGUAJI FULL

UTAMU WA JAMILA FULL