LOML | Love Of My Life (127)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:127
Na Mara nyingi siku hii huwa nachelewa kurudi nyumbani kulingana na kazi zangu huko ofisini. Hivyo hata nyumbani wamezoea na wakati natoka tu Gabriella aliniagiza baadhi ya vitu.

Kwa bahati mbaya ilipofika saa 7 mchana kichwa kilikuwa kinaniuma sana. Ilinibidi nitoke kabla ya muda. Nilipiga simu ya mke wangu nimwambie ili anikumbushe vitu vyake lakini haikuwa inapokelewa na kwakuwa nilikuwa najisikia vibaya nikajiambia nitamnunulia kesho au baadaye tutatoka wacha nikapumzike kwanza.

Nilifika mpaka nyumbani, niliingia sebuleni nikaona simu ya mke wangu, nikachukua na kuweka mfukoni ili nikiingia chumbani nimpatie. Wakati naenda chumbani mama babuu aliniita β€œboss!!”

Nilimtazama na kumuuliza β€œkuna tatizo?”
Mama babuu alishindwa kuongea, macho na uso wake havikuwa sawa. Nilishusha pumzi na kusema β€œsijisikii vizuri baadaye kidogo.”


Nikapandisha mpaka chumbani, nimefika mlangoni nasikia mke wangu anapiga kelele za raha na miguno ya raha. Nilishtuka, Mara nasikia vicheko na maneno sisikii vizuri. Nilijihisi kufa, nilikuwa tayari nimejiandaa kuua siku hii.

Kama ameleta mwanaume chumbani kwangu nitaua. Nilifungua mlango kwa pupa na nguvu zangu zote. Sikuamini nilichokiona, sikuamini nilichokutana nacho.

Niliishiwa nguvu, hata wao hawakuamini kuniona pale muda ule. Mke wangu mimi, aliyeomba msamaha na kuapa kwa Mungu, padri na familia, yeye aliyetaka kujiua ndiyo ameamua kuninyonga kabisa.

Mke wangu Alikuwa anafanya mapenzi tena mapenzi ya raha na Giana wakiwa watupu kitandani kwangu. Najua hujanielewa, nimesema na Giana, shemeji yangu mpole, mwenye hekima, na upendo na bado ni mke wa mtu kumbe yeye na mke wangu ni wapenzi tena wapenzi walioshibana maana sio kwa raha zile.

Nilishindwa kuongea, nilishindwa kuinua mguu, nilikuwa natetetemeka mpaka midomo hata sielewi nifanye nini maana kwa Mara ya kwanza naona wanawake wanafanya mapenzi wenyewe kwa wenyewe tangu nizaliwe.

Tena sio wanawake ni mke wangu na rafiki yake kipenzi ambaye namuheshimu sana na sasa nipo hapa nawaona wakiwa uchi wa mnyama kama walivyo zaliwa ….

πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒIla dunia ya sasa haloooooooo anyway kama unasoma em sema neno hapa maana nachanganyikiwa πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata