LOML | Love Of My Life (129)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:129
Hata kama upo na kila kitu, kama huna ujasiri utadharaulika tu.Wema Bila mipaka, hukaribisha dharau kubwa sana. Ukiendekeza wema utakuwa unakosea kila siku kwasababu watakuumiza tu.

Hata siku moja mapenzi hayabadilishi mtu Bali maumivu, maumivu ndiyo hufanya tujue uwezo wa mtu kitabia.Kamwe huwezi mfurahisha mtu ambaye kwake furaha ina tafsiri tofauti hata yeye mwenyewe hajifurahii.

Wapi watu wanaomba msamaha ili tu waendelee kukuumiza ndiyo wanapenda hivyo.Amani ni gharama sana, Ina chukua akili, moyo, watu wako, na sadaka ya vingi kupatikana.

Gereza pekee gΓΌmΓΌ kulikimbia ni maumivu, maumivu, sio kila Vita ni za kupigana, zingine ni kuweka mipaka tu inatosha. Utahangaika sana Ila mtu anaweza tafuta mbadala wako kwa sekunde tu.

Kitu pekee unaweza kufanya sasa hivi, ni kujisahaulisha kila kitu kwasababu Mipaka yako itawaudhi wote waliozoea kukutumia ovyo. Nakuambia hivi kwasababu nimewahi kuwa kwenye hali kama hii, hali ya maumivu sana.

Najua nimechanganya Ila ukikaa ukatulia utagundua kuwa nilikuwa sahihi. Usiku mwema Rodricky, tafadhali acha kulia na utafute namna ya kutatua tatizo lako na mke wako.”

Machozi yalinitoka tena ya motooooo, nililia na kufunga mlango taratibu, vile nafunga Gabby anaita kwa sauti ya chini sana β€œbabe!!, Mume wangu!!, babe please!!”

Nilikuwa Kama sisikii au napigiwa kelele kwa namna najisikia halafu eti nisimame kumsikiliza yeye. Sikuwa naona hata kama ni mtu wa kawaida.

Unaweza kunisema vile unavyotaka, unaweza kunihukumu vile ninavyotaka lakini Mimi binafsi kama mwanaume, mume, kijana ambaye ninayo hofu ya Mungu nilijaribu, nilipambana kuokoa hii ndoa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

LOML | Love Of My Life FULL