
LOML | Love Of My Life (13)


๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:13
Aliniambia kwa kutania โndugu yangu, bwana harusi muda huu una patikana au hujui kazi ya fungate?โ
Nilicheka na kusema โnisharudi nyumbani ndugu yangu. Mke wangu ana changamoto kazinu.โ
Rafiki yangu alisikitika na kusema โhii mbaya lakini mambo yatakaa sawa au unasemaje?โ
Nilitabasamu na kusema โnaamini hivyo.โ
Rafiki yangu akaniambia โnilikuwa nikusalimie tu ndugu yangu.โ
Nilitabasamu na kisha nilivuta pumzi hata rafiki yangu akaniuliza โRicky, kwema kaka?โ
Nilisema kwa upole โhata sijui nini kinatokea ndugu yangu. Naona kabisa mke wangu simpendi, simuelewi kama naona sio mwanamke wangu ninaye mtaka sipati ile furaha.โ
Rafiki yangu alinisikiliza halafu akaniuliza โupo sawa Ricky?โ
Nilijikuta najilaumu kumwambia nikisema โnilijua tu, nilinua utanilaumu badala uniambie nini kinatokea. Potezea kaka.โ
Rafiki yangu aliniambia kwa upole akisema โNakuelewa Ricky, na wala wewe sio wa kwanza kujihisi hivyo na ndiyo maana nakuelewa. Kitu pekee kwa haraka haraka naweza kusema ni kuwa ipe ndoa yako nafasi kwanza halafu mengine tuonane ili tuzungumze.
Nakuambia hivyo kwasababu, huyo ni mke wako, mmeapa leo kupendana mpaka kifo kiwatenganishe na hakuna sababu rahisi ya kufanya muachane na ndoa haina hata maisha. Ricky jifunze kumpenda huyo mwanamke, sijui utafanya nini ila inatakiwa kuwa hivyo.โ
Rafiki yangu alikuwa sahihi, mbali na hayo ni mama wa mtoto wangu. Haya mawazo ya ajabu sijui hata nimeyatoa wapi. Nilimwambia rafiki yangu โnashukuru sana rafiki yangu, sijui hata ni nini ila naomba nikuahidi kuwa nitajitahidi sana kuipa nafasi ndoa yangu. Leo ni jumapili kaka, nimechoka sana. Nipumzike na kesho kesho kutwa tunaweza kuonana.โ