
LOML | Love Of My Life (133)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:133
Nilijitumia ushahidi kwangu, nikaweka tena simu ile mfukoni na sasa nikawa nainuka nashindwa nakaa. Nilitoa simu yangu tena nilimpigia Pina walau nipate msaada hakuwa anapokea simu yangu kabisa.
Ilinibidi nijikaze hapo natokwa jasho sana. Nilikuwa ninahisi moyo unataka kunitoka maana mapigo yangu ya moyo hayakuwa kawaida mpaak mishipa ya kichwa inanicheza.
Nilimpigia simu rafiki yangu Willy, na yeye pia alikuwa hapokei simu. Niliona nakosa msaada kabisa. Natakiwa kujikaza niinuke mpaka kwenye gari.
Sikuweza kabisa, nilianza kuona kama kanisa linazunguruka. Niliona kama viti vya kanisani vinazunguka. KΔ±la kiti kinazunguka. Nilishindwa kujipambania kabisa. Ni wazi nilianguka hapa na nilijikuta hospitali.
Nilikuwa sina nguvu, nimechoka na namuona dokta ambaye namfahamu. Nilichoka sana. Nikamuuliza βDokta nimefikaje hapa?β
Alinigeukia na kutabasamu akisema βkaka unaendeleaje?β
Nilimtazama nikisema βnipo vizuri kabisa.β
Dokta aliniambia βondoa shaka, rafiki yako alikuleta hapa na ulikuwa dispensary fulani sijajua ipi rafiki yako ana maelekezo yote Ila ndiyo alikuleta hapa ukiwa na hali sio nzuri kabisa.β
Nilishusha pumzi na kusema βyupo wapi?, tafadhali Naomba niitie.β
Dokta alinitazama na kusema βunatakiwa kutulia hapa, hali yako bado sio nzuri kabisa, naomba utulivu.β