
LOML | Love Of My Life (134)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:134
Nilitazama vile nimetundikiwa drips mpaka nachoka. Dokta alitoka na kuniacha mimi nikiwa sielewi kitu. Mara nilimuona rafiki yangu. Nilitabasamu na kusema βkaka, nimefikaje hapa?β
Kaka alinitazama na kusema βnisamehe sana ndugu yangu, ulipo nipigia sikuwa katika Hali nzuri ya kupokea simu.
Baada ya nusu saa nilipopiga ndiyo kuna mama alipokea na kunipa maelekezo kuwa umeanguka kanisani na ndiyo wamekupeleka dispensary na uzuri walianza kukufanyia huduma ya kwanza vizuri kabisa.
Ilinibidi nikutoe huko sasa nikulete hapa. Kaka mimi kimetokea?, kwani shida ipo wapi?, kwanini unateseka namna hii.β
Nililia, nililia kwa maumivu nikisema βimefika mwisho kaka, sitaweza kukuelezea kitu chochote kwasasa sina nguvu hiyo kwa maana ni aibu kubwa sana, ni aibu kubwa mno.
Kwa hili sasa hivi sihitaji ushauri, sihitaji mawazo ya mtu yeyote zaidi nimefanya uamuzi wangu. Kaka nataka kumpa taraka mke wangu, naachana naye rasmi sitamani hata kumuona kwenye maisha yangu sitamani.β
Machozi sijui hata kwanini yalikuwa hayawezi kunikauka kabisa. Willy alinitazama na kuniuliza βIna maana kitu kibaya zaidi kimetokea ?β
Nilisema kwa kufuta machozi βmno kaka, mnooo!!, kitu kibaya mno.Kuna mtu anajua nilipo?β
Willy aliniambia kwa upole na huruma sana βhapana, ingawa simu yako imeita sana ni namba ngeni na baba lakini sijapokea nilihisi tu itakuwa una shida mahali hivyo nilikuwa naomba uamke salama kwanza.β
Nilishusha pumzi na kusema βnisamehe sana rafiki yangu, nimekusumbua sana. Naomba nisamehe sana.β
Willy alinitazama kwa huruma, nilimtazama na kusema βkuna mtu muhimu sana, natakiwa kukutana naye, lakini hapokei simu zangu, najua bado sipo sawa lakini niamini natakiwa kuinuka hapa na kwenda kuonana naye, nakuomba sana.β