
LOML | Love Of My Life (135)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:135
Willy alinitazama na kusema βHaiwezekani, jisikilize unavyo zungumza. Dokta amesema una hali sio nzuri huwezi kutoka hapa na sasa ni usiku sana. Saa 9 usiku hivi unanielewa kaka. Tafadhali nakuomba vumilia asubuhi kisha nipe maelekezo mimi nitamleta huyo mtu hapa.β
Nilimtazama na kumuuliza βunasema kweli utamleta hapa?β
Aliniambia kwa upole βunatakiwa kupumzika acha kuzungumza sana kaka.β
Nilimtazama na kusema βna wewe nyumbani, fanya uende.β
Rafiki yangu aliniambia βusijali, nimezungumza na mke wangu, hana shida kabisa na mimi kuwepo hapa kukusaidia. Kesho nikimaliza kazi yako tena asubuhi sana nitaenda nyumbani. Haya nipe kwanza maelekezo.β
Basi nilimpa namba rafiki yangu, nilimpa na jina la mahali na sehemu hiyo na kisha namna ya kumpata. Halafu nikampa na jina la Pina. Alinitazama na kuniuliza βni nani hata una mtafuta namna hii?β
Nilimtazama na kusema βnisaidie kaka, acha maswali muda ukifika utajua kila kitu.β
Kaka Willy alinishika mkono kwa upendo akinitazama huku akinitaka nitulie. Kiukweli hali yangu bado haikuwa nzuri. Sikuwa najisikia vizuri kabisa, nilikuwa najisikia vibaya sana.
Nililala, Willy alikuwa na mimi hapa. Hatujakua pamoja, hatujazaliwa pamoja, hatufanyi kazi ofisi moja. Ni mtu ambaye tu tulikutana mazingira ya kazi, nikamuamini anaweza kushirikiana na mimi kazini kwangu na kuniletea wateja.
Ana heshima na nidhamu ingawa ni mkubwa kwangu, zaidi ananiona kama ndugu yake. Ananisaidia sana kusema kweli ninampenda sana kama sehemu ya familia yangu. Ni mtu mzuri sana, namshukuru sana Mungu kwaajili ya uwepo wangu kwenye maisha yangu