
LOML | Love Of My Life (136)


𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:136
Ilikuwa saa 12 nakumbuka niliamshwa na nesi, hata nikamuuliza “saa ngapi sasa?”
Akanitazama na kusema 12:45. Nilishusha pumzi, nesi aliniuliza “Unaendeleaje sasa kaka?”
Nilimtazama na kusema “sijui nesi, nimechoka sana. Nafikiri nahitaji nguvu zaidi.”
Nesi aliniambia “usijali kila kitu kitakuwa sawa, usihofu.”
Nilishusha pumzi na kisha nesi alianza kunipatia dawa, wakati ndiyo nesi anatoka tu, mlangoni nilishangaa kuona anaingia Pina. Nilijikuta napata nguvu, na Pina alikuwa na sura yenye hofu na wasiwasi sana. Nilijikuta naita “Pina!!, Pina upo hapa?”
Willy alimsaidia Pina kwa kumuongoza hata alinifikia kunipapasa na kunikumbatia kwa upendo kabisa akisema “ninajisikia vibaya sana kwasababu sikupokea simu pindi ulinihitaji, nisamehe sana.
Ninajisikia maumivu sana ndani ya kifua changu. Pengine ningesaidia na sasa usingekuwa hapa. Pole sana Ricky, niambie unajisikiaje, unaendeleaje?
Nilimtazama nikisema kwa kutia huruma “Usijali Pina, muhimu ni kuwa upo hapa sasa ninayo furaha sana. Vipi lakini na wewe upo sawa?”
Pina alinitazama, kisha kaka Willy alisogeza kiti na kumsaidia Pina aketi. Na yeye alisema “naenda kufuata Supu kaka, unatakiwa kula.”
Nilisema kwa upole “nashukuru sana kaka, Mungu akubariki sana.”
Wakati huo simu yangu ilikuwa inazidi kuita, niliamua kuizima tu kwanza natakiwa kuzungumza na Pina. Pina alinishika mkono wangu na kuniuliza “shida ni nini?, kitu gani kimekutokea Ricky.”
Nilivuta pumzi na machozi yakawa yananitoka tu, Pina aliniambia “hapana kama hujisikii kuniambia usiniambie tafafhali mpaka ukiwa tayari. Pona haraka tafadhali.”
Nilitabasamu kumuona pale, namna anajali na kuzungumza na mimi kwa upendo sana.Nilikuwa namtazama, na yeye akijali kuangalia nilivyokuwa naendelea, akinishika shingo, mara ananipapasa mpaka kifuani mimi namtazama tu na aliniuliza “tatizo nini haswa?”