
LOML | Love Of My Life (138)


๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:138
Nilikuwa najisikia vibaya sana lakini Pina alikuwa hapa ananilisha hata nilijikaza kunywa Supu. Ingawa sikumaliza ila nilipambana sana kunywa. Baada ya hapo nilishukuru nikisema โnashukuru sana, Ubarikiwe sana Pina.โ
Pina alitabasamu na kusema โunatakiwa kujikaza na ule vizuri ndiyo utapata nguvu ya kuinuka hapa.โ
Willy yeye alitoa vyombo na kisha alisema โPina, mimi nakuacha. Inabidi nifike nyumbani. Sasa sijui una haraka sana ili baadaye nikurudishe nyumbani au sasa hivi?โ
Pina alikuwa ameshika mkono wangu, mimi wakati nataka kujibu yeye alisema โnitabaki hapa na Ricky, nitakuwa naye hapa. Usijali.โ
Nilijikuta natabasamu hata Willy, alinitazama na kuniuliza kwa kuchezesha midomo โni nani?โ
Nilitabasamu tu, kisha Willy aliaga akisema โbaadaye ndugu zangu. Kukiwa na tatizo nipigieni nitakuwa hapa haraka sana.โ
Kwa kutania nilisema โhata usiporudi.โ
Wote tukacheka huku Willy akisema โsasa hivi eenh, Pina ataondoka huyo utanihitaji.โ
Tulicheka sana ingawa mimi cheko langu ni mdogo mdogo ila nilionekana kuwa na furaha hata kama naumwa.
Nilimtazama usoni Pina nikiwa nimelala pale kitandani, nikashika mikono yake na kusema โthanks for coming, nilitamani sana kupata muda na wewe.โ
Pina aliniambia kwa upole โnisamehe sana kwa tabia yangu mbaya nimekuonesha.Kama kitu kibaya kingekutokea ningeshindwa kabisa kujisamehe. Nisamehe sana Ricky, nisamehe sana. โ
Nilimtazama na kusema โnakuelewa Pina, huna sababu ya kuomba msamaha na upo hapa. Asante kwa ukarimu wako. Nashukuru sana.โ
Alitabasamu akaniuliza โunajisikiaje?โ
Nilimtazama nikisema โnimechoka sana, hutojali kama nitalala si ndiyo?โ
Alitabasamu na kuniambia โmimi nipo hapa, nitakulinda, sitaondoka.โ