
LOML | Love Of My Life (14)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:14
Rafiki yangu aliniambia βsawa kaka, kuwa makini sana.β
Nilitabasamu tu na kukata simu.
Ni maneno machache aliniambia, alinikumbusha kiapo changu na bado ndoa yaani hata wiki haina, bado mwanamke huyu nitaishi naye maisha yote na kuanzisha familia naye. Ni mama watoto wangu, ana mtoto wangu tumboni hivyo natakiwa tu kuwa mpole.
Ndani yangu nilijiambia βnatakiwa kupambania hii ndoa sana, natakiwa kumpenda mke wangu. Hata hivyo mbona ni mke mzuri tu, mwanamke mrembo na mzuri sana. Nahangaika na nini tena. Mungu nisaidie.β
Nilichukua simu yangu na kumtumia ujumbe mke wangu βwifeyβ£οΈ, i love you so very much, all the best mama.β
Nikaweka simu pembeni na kujilaza. Usingizi ulinichukua palepale, na vile nilikuwa nina uchovu sana, nililala.
Muda ulipita sana, nilishtuka na kushika simu yangu kama mke wangu amenitafuta. Hakuwa amenitafuta, nilishika simu yangu na kumpigia mke wangu. Mke wangu hakupokea simu yangu. Nikaweka tu pembeni nikisema βitakuwa ametingwa.β
Niliinuka nikawa naelekea chooni lakini ndani yangu najua kabisa mke wangu muda wote simu kwanini sasa hasemi chochote na wakati nilituma text nzuri tu. Hivyo nikawa najisikia kutokupenda kiasi lakini nilitambua ametingwa.
Niliporudi sasa ndiyo nilikutana na ujumbe wake akisema βI miss you Dadieβ£οΈ, nisamehe nimetingwa kiasi. Nitakukuta nyumbani na pole kwa kuwa mwenyewe. Nakupenda hubby.β
Nilisoma tu na kutabasamu nikisema βmke wangu, mke wangu, she is beutiful. Ricky tulia.β
Nikaweka simu mfukoni na kutoka mpaka sebuleni, hapo nilikutana na huyu mama wa hapa nyumbani aliniambia kuwa chakula tayari. Nami nilimwambia kwa heshima βsamahani mama naweza kupata hapa nikala nikiwa hapa.β