LOML | Love Of My Life (142)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:142
Huyu mwanamke ni muuaji, kwanini wake za watu wanafanya hivi, hawana kuchefuchefu. Kivipi yaani?”

Nililia kwa uchungu hata alinikumbatia, tulilia pale kwa Muda, nilimtazama na kusema β€œuliongea kwa maumivu na kusema unayajua maumivu kwasababu uliwahi kuwa kwenye hali hiyo. Pina mimi ni rafiki yako, na Mara zote ni muwazi kwako. Unaweza kuniamini tafadhali?”
Nilimtazama.

Aliinamisha kichwa chini na kusema β€œRicky ni hadithi ndefu kidogo, lakini nitajitahidi sana kupunguza ili unielewe. Itabidi ule kwanza Kisha tutaendelea. Willy alisha andaa hapa.”

Nilikuwa namtazama tu, basi tulisaidiana kuweka mazingira sawa na kwa upendo alinilisha, mchana huu sikuweza kabisa kujikaza kula nilisema β€œnitakula baadaye tafadhali.”

Pina alinitazama na kusema β€œnakuelewa sana, ila unatakiwa kujikaza.”

Nilitabasamu na kusema β€œNina hamu ya kukusikia Pina, niambie nini kilikutokea?”

Pina alishusha pumzi na kusema kwa upole β€œkwanza kabisa nilikuambia si kuzaliwa hivi, nilikuwa na macho yangu mazuri na nilikuwa naona kabisa.

Maisha yangu yalibadilika Baada ya kukutana na mwanaume huyu ambaye tulipendana sana. Isaack.Hili ndiyo lilikuwa Jina lake.

Na wakati huo nakutana naye, nilikuwa ninayo maisha yangu ingawa hayakuwa mazuri sana. Lakini nilikuwa na kwangu na naishi maana nilikuwa nimeajiriwa kwenye moja ya hospitali binafsi na maisha yalikuwa yanasonga.

Niliweza msaidia bibi yangu kwa mambo ya hapa na pale, maisha yalikuwa yanasonga namshukuru Mungu.

Na niliweza kusaidia watoto kwenye kituo cha watoto yatima ambako na mimi nililelewa huko na kanisa hata kama sio kwa utajiri mkubwa lakini sikuwa kinyonge kwa chochote kitu nilikumbuka nilipotoka maana bila wao nisingekuwa hapa nilipo.

Mahusiano yangu na Isack yalikuwa mazuri sana.Ungeona namna nilikuwa na furaha. Alikuwa very romantic man mwenye huruma sana. Alinifanya nimpende, alinifanya nimuamini na kila kitu. Na sikuwa naona tatizo kwenye hilo kabisa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata