
LOML | Love Of My Life (143)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:143
Muda mwingi tulipenda sana kuwasiliana, mambo ya hapa na pale na nilikuwa nafurahia. Siku moja usiku wakati tunawasiliana alimpost mtoto wa miaka mitatu au minne status na alikuwa akimtakia siku yake ya kuzaliwa.
Niliona pia na kumuuliza โmtoto wetu, na mbona hunambii kama Tuna mtoto.โ
Isack alicheka na kuniambia โinabidi tuzae mimi na wewe sasa huyu ni wakaka na wewe ukileta wako mambo yanakuwa safi kabisa.โ
Nilicheka na kusema โnilijua huyu wangu Kumbe inatakiwa nifanye kazi.โ
Tulicheka sana. Na hii siku ilipita tukiwa tumecheka na kufurahi sana.
Maisha yetu hayakuwa mabaya kusema kweli, Isack alikuwa akiniambia mambo mengi kwa uwaze kabisa mpaka miezi kadhaa mbele nilipokuja kugundua kuwa nina mimba, mimba ya Isack.
Nilimtafuta kwa upendo kabisa, na nilimuomba aje nyumbani kwangu tuzungumze. Wala hakuwa na tatizo, alikuja mpaka nyumbani na nilimuelezea hali yangu.
Isack alifurahi sana, alinikumbatia, alinibusu na kufanya nicheke tu. Nilimshukuru sana, nilimwambia โumenifurahisha sana, nilikuwa naogopa sana nikidhani utanikimbia.โ
Alicheka na kusema โmimi, nikimbie hapana haiwezekani kabisa. Pina utakubali nikuoe?โ
Nilizidi kushangaa sana, Nilitabasamu nikisema โnipo tayari, muda wowote mpenzi.โ
Alifurahia na kunikumbatia kwa nguvu sana.
Mpaka anaondoka pale kฤฑla kitu kilikuwa sawa na muda mwingi sana tulikuwa tunawasiliana kwa upendo kuhusu mtoto wetu anayekuja. Baada ya siku tatu aliniambia โbaby, Nimeongea na familia yangu. Wanataka kukuona.โ
Nilifurahi nikisema โunasema kweli mpenzi?โ
Mpenzi wangu alicheka na kusema โjiandae, pendeza nakuja kukufuata kesho si huendi kazini kesho?โ
Nilitabasamu nikisema โYes Baby, kesho nipo off.โ
Baลฤฑ aliniambia โkama unahitaji chochote ili kesho upendeze utaniambia.โ
Nitataka nini mimi, mimi nilikuwa na furaha tu. Nilikuwa nimefurahi sana.

