
LOML | Love Of My Life (144)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:144
Nakumbuka sana sΔ±ku hii.Baada ya kukata simu usiku ule nilikuwa nina kazi ya kujaribu nguo hii na ile ukitoka hii najaribu hii. Nilikuwa na furaha sana, Nilifurahi mno.
Kulala kwangu kulikuwa kwa taabu sana, Muda wote nilikuwa nawaza naenda ukweni unajua tena raha yake. BaΕΔ± asubuhi niliwahi sana kuamka, niliamka mapema sana. Nikafanya usafi, nikampigia baby wangu kumuuliza anakuja muda gani na yeye aliniambia mida ya saa 6 atakuwa amefika pale.
Nilikuwa naona saa 6 ni mbali, muda wote nawaza naenda kuona baba na mama wa Mwenzangu ambao watakuwa ni baba na mama yangu pia kwa maana mimi Sina wazazi.
Nilikuwa hata najipa vikazi vya hapa na pale ili mradi tu muda uende, Muda usogee na hilo likafanikiwa mpaka ilipofika saa 6. Kweli ndani ya hiii saa mpenzi wangu alifika.
Haraka nilijiandaa, Hakika nilipendeza sana, alinitazama na kusema βumependeza sana, mke wangu unajua wewe ni mzuri sana.β
Nilitabasamu na kusema βwazazi bila Shaka watapenda.β
Mpenzi wangu alisema βsanaaaa.β
BaΕΔ± alikuwa na gari yake akanichukua mpaka nyumbani kwao. Palikuwa pametulia sana. Binafsi nilifurahia sana kupaona. Alinishika mkono na kusema βkaribu sana nyumbani Pina.β
Nilitabasamu na kusema βnashukuru sana, Ubarikiwe sana Mpenzi.β
BaΕΔ± tuliingia ndani, nilikaa sebuleni nikishangaa picha za ukutani na mpenzi wangu alienda kuita familia yake. BaΕΔ± kuna mwanamke alitoka, nilipomuona nilisimama na kumsalimia kwa heshima zote.
Alikaa na alikuwa ananitazama. Namna ananitazama binafsi sikuona upendo hata niliogopa. Wakati huo binti mwingine alitoka, ambaye tulilingana fulani, tulisalimiana na Kisha Baada ya hapo Mimi nilikuwa tayari akili imenicheza.