LOML | Love Of My Life (145)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:145
Familia haikuwa imenipokea kwa furaha kabisa naona kwenye sura zao. Mama huyu alinitazama na kusema “Isack kwa hiyo huyu ndiyo unataka kumuoa.”

Isack alinitazama na kusema “ndiyo mama, anaitwa Pina ni mwanamke mzuri sana kuwahi kutokea kwenye maisha yangu.”

Huyu mama na binti yake walitazamana na Kisha huyu mama akasema “kwahiyo huyu ndiyo atakuwa mama wa kambo wa mjukuu wangu, una Hakika atakuwa mama wa mambo mzuri kwa mjukuu wangu?”

Nilishtuka hata Isack alishtuka na kunitazama. Halafu akaita “bibi I!!, bibiiii!! Njoo bibi yangu.”
Alikuja mtoto wa kiume ambaye mimi huwa naona mpenzi ana Mpost na Kisha huyu mama alisema “bibi yangu,huyo hapo ndiyo mama yako wa kambo sasa, msalimie.”

Mimi hapo nilikuwa nashangaa hata mama huyu alisema “au hajakwambia ana mtoto?. Wewe Isack inakuaje hujasema una mtoto. Kama ulikuwa hujui huyu ndiyo mjukuu wangu wa kwanza kwa Isack. Na wewe ndiyo utakuwa mama wa kambo utaweza binti?”

Unajua kama ugomvi, mimi hali tayari nimechukia kwanini mpenzi wangu hakuniambia na tayari nilimuuliza akasema ni wa kaka yake. Kiukweli alinikera Sanaa. Ila nitafanyaje, ilinibidi niigize pale nikisema “Hujambo mtoto mzuri?”

Mtoto huyu alinitazama tu, na Kisha mama mkwe alisema “Karibu sana, hapa ndiyo nyumbani kwa Isack. Mimi ni mama yake. Karibuni sana. Mimi naenda zangu kupumzika.”

Nilishangaa sana, Nilidhani labda tulihitaji kufahamiana zaidi. Na Kisha mama huyu alisema “Naenda kupumzika msiniamshe jamani.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata