
LOML | Love Of My Life (147)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:147
Nakuomba sana usimzingatie mama atatuumiza tu. Muhimu tufanye mambo yetu. Akitaka kuungana na sisi sawa, ila suala na nisikuoe kΔ±sa yeye hakutaki sikubaliani nalo kabisa.β
Nilivuta pumzi na kusema βnaogopa sana Isack, kwanini mama ananichukia namna hii mimi na wala sijawahi kumkosea.β
Isack alinitazama na kuniambia βMpenzi, muhimu tumefanya ya muhimu sasa tuendelee na mambo yetu.β
Nilimtazama kwa upole na kusema βkama ni hivi basi hakuna haja ya sherehe, maana Mimi sina familia na wewe familia yako ndiyo Kama hii. Tufunge ndoa na tipiΔe picha maisha yaendelee.β
Isack alinikumbatia akisema βmimi Nakupenda sana, na nitafanya lolote unalotaka suala la muhimu Ia muhimu ni kuwa wewe ni mke wangu.β
Nilitabasamu tu.
BaΕΔ± maisha yalianza hata sasa tulianza kufuata mafundisho ya ndoa kanisani. Siku ya kwanza tu nimeanza mafundisho usiku wake niliota ndoto.
Niliota ni siku ya ndoa yangu, siku hii nilichelewa sana kuamka, mtu wa makeup na yeye hakufika kwa wakati. Nilikuwa chumbani kwangu na mama yangu ambaye alikwisha fariki muda mrefu sana.
Nikawa nalalamika nikisema βmama, nimechelewa sana kuamka, nimechelewa kanisani sasa itakuaje na mpaka sasa mtu wa make up hajafika.β
Mama aliniambia kwa upole βtulia mwanangu, atafika sasa hivi eenh.β
Wakati anasema hivyo mlango uligonjwa ndiyo mtu huyu wa makeup alikuwa anafika. Nilianza kumwambia afanye haraka nishachelewa. Baada ya hapo nikamwambia mama yangu βmama fungua basi hilo shela, inatakiwa nipendeze sana leo.β
Mama yangu alifungua na Kisha alitoa gauni. Nilishangaa sana kuona hili gauni, lilikuwa ni shela zuri sana ila Jeusi. Hakuna hata urembo wa rangi nyingi ni jeusi kila sehemu. Mama βumeona sasa gauni lako zuri sana.β
Nilishangaa na kusema βmama ni jeusi, shela jeusi kwanini nivae nyeusi wakati utaratibu ni nyeusi.β
Mama alinitazama na kusema βmwanangu unatakiwa kuwa wa tofauti eenh, ukawe na nuru kuliko wote tafadhali vaa unachelewa.β