
LOML | Love Of My Life (148)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:148
Nilimtazama mama na kusema βAcha utani mama, siwezi kuvaa nguo nyeusi kabisa kama hutaki tuongozane mpaka madukani sawa ila mimi kama mimi sitavaa shela jeusi.β
Mama alinitazama na kusema βmwanangu madukani tutachelewa vaa tu hili mbona zuri tu.β
Nilikuwa naona kama mama ananitania vile. Nilikuwa hata nalia machozi nakagua lile gauni. Nikiwa napambana niende sokoni simu yangu ilinishutua, ndiyo iliyoniamsha. Kutazama hivi alikuwa ni mpenzi wangu.
Tulizungumza kutakiana asubuhi njema na Baada ya hapo nilijikuta najiuliza βmama yangu na gauni jeusi ni nini tena?, itakuwa ni ndoto tu. β
Nilishuka na kujiandaa kwenda zangu kazini. Nilinyamaza kimya wala sikumwambia mtu yeyote Yule. Hata mpenzi wangu sikumshirikisha ndoto hii. Maisha yakaendelea.
Ilifika tena jumamosi siku ya kwenda kwenye mafundisho ya ndoa. Kila kitu kilikuwa ni kizuri kabisa, hata Baada ya mafundisho mimi na mpenzi wangu tulienda mahali kula.
Nakumbuka usiku huu tena niliota ndoto Kama ambavyo niliota ile siku, lakini safari hii gauni ilikuwa nyeupe nzuri sana. Lakini Baada ya kulivaa tu lilionekana kuwa limetobokatoboka sana. Halifai kabisa ni kama gauni La kale hivi hata nashindwa kulielezea.
Na siku hii nilikuwa na bibi yangu. Bibi yangu ananishangaa ananiambia βhivi mjukuu wangu gauni imepatwa na nini?, bado masaa tu ndoa yako ifungwe. Nakuomba mwanangu, tufanye tu namna ingine tupate gauni.β
Sasa mimi namuuliza bibi huku nalia sana, βbibi yangu, inakuaje sasa, Muda umeenda sana bibi, tunafanya nini sasa Ina maana sitafunga ndoa na Isack. Bibi unajua kabisa haitakiwi kuwa hivyo.β
Bibi alisema βIsack atakuoa lakini mjukuu wangu, sasa itakuaje na hii nguo?β