LOML | Love Of My Life (150)

๐‹๐Ž๐Œ๐‹ (๐‘ณ๐’๐’—๐’† ๐’๐’‡ ๐’Ž๐’š ๐’๐’Š๐’‡๐’†) โฃ๏ธ:150
Bibi yangu alisema kwa upole โ€œmjukuu wangu unatakiwa kusali sana. Maana sielewi hizi ndoto Zina maana Gani, tuingie kwenye maombi.โ€
Nilimwambia bibi yangu โ€œnafikiri upo sahihi bibi, tuingie kwenye maombi.โ€

Bibi yangu alikuwa ananitazama hata namuuliza โ€œmbona unanitazama sana? โ€œ
Bibi akaniuliza โ€œkwani mjukuu wangu, ni sawa umekosea tayari kwani ni lazima uolewe na Isack kwasasa.โ€

Nilimtazama nikitabasamu na kusema โ€œbibi unaongea nini. Bado wiki chache sana na tayari Tumeanza mafundisho.โ€
Bibi alinitazama akisema โ€œNakutegemea mwanangu, roho yangu haina Amani kabisa. Lakini Mungu atatusaidia.โ€

Nilimtazama bibi na kumwambia โ€œbibi usijali mimi na Isack tunapendana. Nitasimama na Mungu na Mungu atatusaidia sana.โ€

Bibi alikuwa anatabasamu tu. Siku hii nilishinda na bibi yangu hapa. Mpaka jioni Isack alinifuata kwa upendo. Alisalimiana na bibi kwa furaha akampa na pesa. Mimi na bibi Tuliagana huku bibi yangu akisisitiza sana juu ya maombi.

Nilifika nyumbani na Isack alilala hapa siku hii kesho yake alinipitisha kazini na Kisha yeye akaendelea na mambo yake na siku hii Mimi ndiyo nilianza kufunga na kuomba.

Ukifika muda wa kuomba naingia chooni narudi naendelea na kazi. Tangu nianze kuomba maisha yangu yalikuwa rahisi sana. Sikuwahi kuota tena ndoto mbaya. Hata Mara moja sikuota kuhusu harusi. Maandalizi yalikuwa mazuri tu mimi na mume wangu mtarajiwa na hata nguo na viatu tulipata vya kupendeza sana.

Nakumbuka usiku kabla ya harusi ndiyo niliota hii ndoto. Niliota nipo chumbani na mama yake Isack. Nimependeza sana hata yeye anasema โ€œunajua mkwe wangu wewe ni mzuri sana, umependeza sana mwanangu.โ€

Nilitabasamu tu, Kisha nilimtazama mama na kusema โ€œnaomba viatu mama.โ€

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata