
LOML | Love Of My Life (151)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:151
Huyu mama aliniletea kandambili, kubwaaa, chafuuuu, chakavuuuuu mpaka nyingine imekatika. Na hizi kandambili ni tofauti moja nyekundu nyingine ni blue na nyingine imekatwa mbele nyingine nyuma. Ni chafu sana, ni chakavu sana hata nilimtazama mama mkwe wangu na kusema βmama nataka viatu sasa mbona kandambili?β
Huyu mama alianza kucheka na kusema βviatu?, Hakuna kuvaa viatu wewe leo ni utavaa kandambili ndiyo zinakutosha. Tena utavaa lazima maana muda umeisha si unaona.β
Nilianza kulia nikisema βhaiwezekani, haiwezekani kabisa.β
Vile nazungumza hivyo nikilia mlango uligongwa. Nikashtuka sana. Nilipoenda kwa kujivuta sana kufungua alikuwa ni rafiki yangu na bibi yangu wamekuja nichukua niende saluni. Lakini macho yangu yaliendelea kuonesha kama nilikuwa nalia hata niliulizwa βmbona unalia?β
Nilijibaraguza tu na kuwaomba wanisubiri nijiandae ili tuondoke.
Nilikuwa Sina furaha kabisa. Nilipambwa vizuri, nikapendeza vizuri na gauni yangu lakini ajabu kiatu ambacho kilikuwa kinanitosha vizuri tu kikawa kinanivuka. Hata nikawa nashangaa mbona kiatu kimekuwa kikubwa tena.
BaΕΔ± watu wa saluni wakawa wananiwekea mpaka na tishu ili kinitoshe lakini wapi. Nilijikuta naumia sana ndani ya moyo wangu. Lakini Mpenzi wangu alikuwa na mimi, alikuwa na mimi kΔ±la mahali alinipigia na kunitia moyo Mara kwa mara.
Muda wa kwenda kanisani ulifika, hii siku badala ya kuwa siku ya furaha ikawa siku ya huzuni maana tulikuwa mimi na mume wangu na wasimamizi halafu rafiki mmoja wa Mr na na rafiki yangu mmoja tu na Kisha bibi yangu.
Hakuna ndugu hata mmoja ambaye alitoka familia ya mume wangu sio mama, sio baba, sio Wifi wala kaka zake. Walitususia shughuli. Kanisa ni jeupe ni waimba kwaya tu na sisi. Hii ilimkata hata mume wangu, hata alikuwa analia tu.