
LOML | Love Of My Life (153)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:153
Huyo Faraja sasa ndiyo mzazi mwenzake na mume wangu. Nilishangaa inakuaje wana ukaribu namna hiyo, alikuja pale na mama alisema βumemuona mke mwenzio sasa, sio mwenzako anakuja kwako kumuona mtoto au kuchukua mtoto unavimba. Umemkuta huyu, na ndiyo mwanamke wa kwanza wa Isack.β
Isack akasema βmama ni nini lakini?β
Mama alisema βkalete chakula binti yangu.β
Mimi hapo machozi yananitoka natamani kuinuka siwezi. Siwezi kwasababu mume wangu ananizuia. Machozi yanatamani kunitoka.
BaΕΔ± huyo Faraja kaandaa chakula, nikawa kama nisile lakini mume wangu akawa ananishauri nile. Nikachukua tu kidogo hata mume wangu alisema βongeza chakula mke wangu.β
Nilimtazama na kusema βkinatosha mume wangu.β
Wifi yangu akasema βtangu lini bibi harusi akala sana mwisho anenepe vidole pete zisimtoshe.β
Halafu walicheka sana. Hata mume wangu alishindwa kuvumilia aliniinua akiwa amekasirika na tuliondoka huku mama akiita huku anacheka βwewe Isack, Isack Acha ujinga rudi hapa, wewe mpuuzi rudi nimesema.β
Mimi nilikuwa nalia tu namna wananikejeli. Hata mume wangu aliniambia βpole sana mke wangu, unatakiwa kujikaza.β
Nilimtazama nikisema βkivipi Isack, hawanipendi, hawanitaki na inakuaje faraja yeye ndiyo yupo pale Ina maana ndiyo anapendwa sana una uhusiano naye gani?β
Mume wangu alikana, alisema uhusiano wao umeisha zamanΔ± na ndiyo maana amenioa mimi.Nilikuwa naendelea tu kulia. Roho yangu ilikuwa inaumia sana kusema kweli. Kukataliwa ukweni inauma sana, inatesa sana maana kuna watu wanatabia za kuumiza na kutesa sana.
Nilimwambia mume wangu βIsack Nakupenda sana, lakini kwa namna naona haya maisha Naomba niwe mbali na familia yako, sitaki kuwa karibu na familia yako kamwe.β