LOML | Love Of My Life (154)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:154
Mume wangu alinitazama na kusema “nakuelewa mke wangu, hata mimi naumia sana. Natamani familia yenye furaha sana.”
Nilimkumbatia mume wangu na tulianza kurudi nyumbani nikiwa sina raha kabisa.

Sikuwahi kurudi tena kwao, na Mimi mimba yangu ikawa Inakua. Nakumbuka zilipita siku, mimba nayo ikawa inasumbua ilinibidi nisimame hata kazı hospitali. Nikawa tu mtu wa nyumbani, mume wangu pekee alikuwa msaada na bibi yangu kila aliponitembelea.

Nakumbuka miezi mitano hivi ya mimba yangu siku hii mume wangu alikuja na mama yake na mtoto wake. Niliwapokea vizuri ingawa moyoni Nilishangaa.

Mama alinitazama na kusema “mwanangu kuwa na Amani, mume ameniambia mimba inakusumbua sana nikaona nije nikuone. Wewe ni mwanangu na mimba ni ya mwanangu kipenzi siwezi kukuacha peke yako. Mengine tuyaache nyuma sasa ni afya yako mpaka mtoto azaliwe. Sawa mwanangu.”
Nilitabasamu na kusema “nashukuru sana mama, karibu.”

Başı nilijikaza nikaaandaa chakula, mama huyu sıku hii alikuwa na furaha. Alisifia chakula hata akasema atakuwa anakuja mara kwa mara kuniona na aliniambia kuna dawa ni nzuri sana kwa wajawazito kwaajili ya vijicho na kujifungua salama na mambo Kama hayo huku akisema “hata mke mwenzio mke wa shemeji yako na yeye sasa amejifungua salama kabisa hiyo dawa ni nzuri sana. Hizi homa zote zitaisha.”
Mimi nilitabasamu tu.

Başı siku hii akaosha vyombo, akasafisha nyumba na aliaga na furaha sana akamuacha mjukuu wake hapa akisema “muangalie mama, mimi nitarudi nikipata tu hiyo dawa ndiyo tutaondoka wote. Mlinde mama yako eenh.”
Mtoto anatabasamu tu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata