LOML | Love Of My Life (155)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:155
Nilimtania mume wangu nikisema β€œalichokula leo ale kila siku.”
Mume wangu alicheka akisema β€œnilikuambia mimi, mtakaa sawa tu. Wee subiri.”
Mimi Nilicheka tu.

Nilikaa na mtoto huyu vizuri sana. Tulikula pamoja nilinunua nguo kwaajili yake. Tulitoka pamoja sikuweka kinyongo chochote ndani ya moyo wangu. Nilikaa kama siku tano, huyu mama Mkwe alirudi na dawa.

Alinipikia Tukala na alihakikisha nakunywa dawa vizuri. Na jioni aliaga na mjukuu wake akisisitiza niwe nakunywa na yeye kila atakapokuwa anapata ataniletea. Kusema ukweli dawa ilikuwa inanisaidia sana.

Homa zote zilikata, nilianza kula vizuri hata mwili ukaja. Nilikuwa namshukuru sana mama mkwe wangu na alianza kunipigia simu kuniuliza naendeleaje. Hakika wakati wa mimba niliona mabadiliko makubwa sana.

Hata ilifika sΔ±ku ya kujifungua. Mume wangu alikuwa na mimi, hospitali sikuona mtu mwingine zaidi ya mume wangu na bibi yangu. Mungu alinisaidia nilijufungua mtoto mzuri wa kiume. Tulifurahia sana. Hata mume wangu aliniambia β€œsasa mke wangu inabidi uende nyumbani kwa mama.”

Nilimtazama na kumuuliza β€œIna maana hawajui nipo hapa mbona hawajaja?”
Mume wangu alisema β€œmke wangu Acha malalamiko, unatakiwa kufuata ninachosema.”

Nilimtazama tu ila sikutaka mimi nilitamani tu nikae kwangu na bibi yangu. Lakini mume wangu ndiyo kaamua. Ikawa hivyo. Nimefika pale hakuna hata mtu ana kuja kumshika mtoto.

Mume wangu kaondoka nipo mwenyewe. Mtoto analia na mimi nina mshono tena mbichi nambembeleza mtoto mpaka nalia. Siku hii nilitamani mama yangu angekuwa hai. Nililia sana na mtoto analia.

Usiku mtoto halali na nikapata tumbo La kuhara lakini wapi pamoja na kutoka kote kwenda chooni Hakuna mtu hata alikuja kuniuliza. Muda wa karibia na asubuhi ndiyo nilipata usingizi.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

TOBO LA PANYA FULL

SIMULIZI YA INGIZA FULL

CHAGUO LA MOYO FULL