LOML | Love Of My Life (157)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:157
nitese utakavyo ila mimi nikiwa na wewe. Siogopi kuumia na wewe Pina.

Hata kama sio sasa, wakati unafikiria kuwa na mahusiano basi niwepo kwa maisha yako ili niwe wa kwanza kupata nafasi hiyo. Nakupenda sana, Nakupenda Pina.

Know that, nakupenda. Sipendi kuona unaumia hivyo sitamani kukumiza. Naomba tuunganishe maumivu yetu na tupone pamoja. Nasikitishwa na simulizi yako, ila ninayo imani tutapona pamoja.”
Pina aliniita β€œRodricky!!!”

Niliinua mkono wangu na kushika mashavu yake, nilikuwa nampapasa, na yeye alinishika mikono yangu kwa upendo akitokwa machozi. Ghafla mlango ulifunguliwa, nilishangaa kumuona mama yangu, na Gabriella bula hata aibu.

Mama alinikimbilia na kunikumbatia. Wakati huo Willy anamsaidia Pina. Kama alisema β€œmwanangu, kwanini unanifanyia hivi eenh, sasa mbona hujaniambia chochote na umekaa siku zote hizi?”

Nilimtoa mama mwilini na kusema β€œMama huyu shetani amefuata nini hapa?”
Mama alishangaa, na kusema β€œmwanangu huyu si mkeo Gabriella.”

Nilijikuta napata nguvu nilikaa na kusema β€œmke wangu kwa ndoa ipi mama, mimi na Gabriella tumemalizana. Sitaki kuona hata sura yake popobawa mkubwa huyu.

Naomba umtoe hapa mama, mtoe na sitaki kumuona kwangu. Aondoke kabla sijapata kesi mbaya. Sikutaki na kamwe usikanyage hapa.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

TOBO LA PANYA FULL