
LOML | Love Of My Life (16)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:16
Niliamua kulala, mke wangu alipotoka aliita βHubby!!, Hubby maskini ushalala, pole mpenzi.β
Akanibusu na kuendelea na mambo yake. Nilimuona akichukua simu yake akatoka na chumbani kwenda kuzungumza nje.
Kiukweli ndiyo ndoa Ina siku moja tu Ila naona inanisumbua, lakini ndani yangu nasikia sauti kuwa βunawaza nini lakini Ricky, Gabriella ana matatizo na ana jitahidi kushughulikia na kuweka sawa mambo tafadhali muelewe.β
KΔ±la nilipo Waza hivyo walau moyo wangu ulitulia.Niliendelea kulala tu.
Asubuhi niliamka kwa kuchelewa, lakini nilipo amka mke wangu hakuwepo kitandani. Na badala yake nilikutana na ujumbe tu mezani. βHello mume wangu, nimekuacha upumzike. Leo sitachelewa kurudi nakupenda sana.β
Nilisoma tena huu ujumbe, uliishia kunikwaza tu. Hata nilisema βjana amerudi Hana muda kabisa na mimi, leo tena amewahi kuondoka na kuniacha hapa ina maana kazi ni Bora sana kuliko mimi au kuna kitu sielewi nakuza.β
Nilijiuliza, baadaye nikachukua simu yangu na kumpigia rafiki yangu, rafiki yangu jina lake ni Willy. Willy alipokea simu, nikamuuliza βupo wapi kaka tuonane.β
Willy aliniambia βNipo kwangu kaka, karibu.β
Nilimwambia βnakuja kaka, nakuhitaji sana wakati huu.β
Willy alinikaribisha kwake kwa upendo sana.
Basi nilijiandaa vizuri na nilipotoka nilikuta chai imeandaliwa nami nilikunywa hapa na kuagana na huyu mama hapa kwa upendo kabisa. Nilichukua gari yangu na kuondoka zangu.
Niliendesha gari mpaka nyumbani kwa Willy. Mimi na Willy tunaonana sana nje ya nyumbani hii ndiyo mara ya kwanza nafika kwake. Alifurahi sana kuniona, hata anilikaribisha akisema βkaribu sana kaka hapa ndiyo nyumbani. Karibu sana. Sasa niambie tutakaa nje au ndani?β