
LOML | Love Of My Life (162)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:162
Mungu akinipa nafasi ya kuendelea kuishi, na kupenda basi nimefungua moyo wangu, kwaajili ya mwanamke mmoja tu. Pina mama, Pina peke yake sitajali lolote kwasababu moyo wangu unamtaka yeye tu.
Mama yangu alinitazama na kusema βnisamehe sana mwanangu, najua, nakuelewa pengine mimi sio mama mzuri kwako. Nakuahidi nitajirekebisha. Lakini kamwe mwanangu, kamwe sitakubali hata mara moja uwe karibu na yule binti.
Hamfanani, unataka familia ya watu wasioona, unataka umaskini maana ipo wazi ukijihusisha na maskini na wewe unakua maskini, ukijihusisha na kipofu na wewe utakuwa huoni.
Labda nife mwanangu, sitakubali hata mara moja mahusiano na yule binti, eti ndoa yako inasumbua halafu yule mshamba ndiyo awe mkwe wangu mimi, labda niwe nimekufa.β
Nilimtazama mama yangu, alikuwa ananikera tu. sikuwahi kujua kuwa mama yangu na yeye ana roho mbaya namna ya kujali vitu kuliko utu. Nilikuwa namtazama vile anapiga kelele zake na alipo maliza nilisema βunaweza kutoka mama.β
Mama alishangaa na kuniuliza βunasemaje?β
Nilirudia tena βnataka utoke, ninahitaji kubaki mimi mwenyewe naomba utoke hapa.β
Mama aliniuliza βhivi upo sawa?, naona unasahau mimi ni mama yako?β
Nilimtazama na kusema βukijihusisha na wapumbavu?β
Mama alingβaka akisema βumekosa adabu namna hii, kwahiyo unataka kusema mimi ni mpumbavu?β
Nilimtazama na kusema kwa hasira βmama acha maigizo, sihitaji kelele mahali hapa. Ndiyo maana nilikuambia hujali kuhusu mimi, unafurahia maumivu yangu. Ondoka hapa, ondoka mama.