LOML | Love Of My Life (163)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:163
Mama alibeba mkoba wake kwa hasira na kutoka. Nilibaki nimekasirika sana. Nilikasirika kwa maneno ya mama yangu. Alivyo zungumza kuhusu Pina, na namna anataka mambo yawe.

Lakini baada ya kukumbuka maneno ya Pina. Busu lake nilitabasamu. Na wakati huo dokta alikuwa anaingia. Niliendelea kutabasamu hata akasema “naona una furaha sana.”

Nilitabasamu na kusema “maisha yananipa sababu ya kutabasamu kwa mara nyingine.”

Dokta alitabasamu na kisha aliendelea na kazi yake na kusema “ulikuwa unaendelea vizuri, kwasasa naona hali yako imebadilika tena. Sikia nikuambie kitu Rodricky, unatakiwa kutulia kabisa ili hali hii ikae sawa usifanye masihara tafadhali sio nzuri.”

Nilivuta pumzi na kusema “nimekuelewa tafadhali, nitakuwa makini. Naomba ukitoka hapo niitie Pina na Willy.”
Dokta alinitazama na kusema “Pina sijamuona. Willy yupo.”
Nilishtuka, huku moyoni nikijiuliza “ina maana ameondoka?”

Nilitamani kujua hili kutoka kwa Willy. Dokta alimaliza mambo yake na kisha alitoka. Alipotoka tu haukupita muda sana Willy aliingia ana tabasamu. Sikuacha hata amalize kutabasamu nikamuuliza “Kaka Pina ameondoka?”

Willy alinitazama na kusema “kaka kile chuma umetoa wapi?”
Nilimtazama na kusema “una maana gani?”
Aliniambia “niahidi utanisimulia kila kitu kuhusu yeye. Sio poa, amenyooka hivi, haogopi na hapo ni haoni lakini Mungu wangu!!, Mungu wangu!!!”
Nikamuuliza Willy “acha mafumbo, niambie nini kimetokea?”
Alishusha pumzi na kusema “baada ya kutoka hapa, alionekana hana raha hata nikamuuliza kama yupo sawa. Alinijibu tu nisijali yupo sawa.

Baada ya muda mkeo alitoka analia, na moja kwa moja alikuja mpaka kwa Pina. Sasa si unajua Pina haoni, mkeo alianza kupiga kelele zake na tambo nyingi akimtaka Pina akae mbali na wewe.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata