LOML | Love Of My Life (166)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:166
Atakuwa ana maanisha?. Amesema atamuonesha namna natakiwa kupendwa na kuheshimika. Maneno yake kaka, yupo wapi kwani?”

Willy alivuta pumzi na kusema β€œbaada ya kumshika shemeji atoke nje, alikuwa anasema sitakubali hili, nitakuonesha hiyo 10 inakuaje, wewe si unajiona kichaa, siwezi kuacha unamchezea mume wangu, nitakuonesha.”

Wakati huo na mama yako alikuwa anatoka, alimfikia Pina na kumvuta bila hata kutaka maelezo nikawafuata nyuma. Walisimama nje ya hospitali na sijui wanaongea nini.

Nilimwambia Willy β€œnamfahamu mama yangu, naomba umfuate tafadhali mwambie namuhitaji.”
Willy alinitazama na kusema β€œhalafu utaniambia?”

Nilitabasamu na kusema β€œkila kitu, niitie kwanza.”
Nilitabasamu tu na Willy alitabasamu. Alikaa huko kwa muda huko aliponfuata wakati huo mimi nikikumbuka sakata la Pina na Gabby nacheka, Pina ni jasiri sana nilijikuta natabasamu, na vile vibao ndiyo kabisa na kisha akarudi akiwa peke yake.

Nikamuuliza kwa kumshangaa β€œVipi mbona peke yako?”
Alinitazama na kusema β€œamenipenda mwenyewe, amenifuata mwenyewe tatizo sio mimi hapa, tatizo ni kijana wako. Ongea naye mwambie aniache akiweza nitamuacha kama hawezi mama itabidi unipokee kama binti yako kipofu hapo vipi mama.”

Nikamtazama Willy na kusema β€œndiyo nini?”
Willy alisema β€œndiyo Pina amemwambia mama yako hivyo?”
Nilijikuta nacheka nikisema β€œeenh Bwana eenh?”

Willy alisema β€œusicheke, anaumia, yupo nje hapo analia, anajikaza tu lakini wanamwambia maneno mabaya sana.”
Nilijikuta najisikia vibaya na kusema β€œnaomba niitie tafadhali, nahitaji kuzungumza naye.”

Kabla Willy hajaamka, Pina aliingia na kusema β€œnipo hapa Rodricky.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BINTI MDUNGUAJI FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

KIBOKO YANGU FULL