
LOML | Love Of My Life (167)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:167
Niliita βPina upo sawa?β
Pina alisogea kidogo, kisha alinifuata mpaka nilipo na alisema kwa upole βnisamehe sana kama nimekosea kwa mama na mkeo. Nilitaka ujisikie vizuri, nilitaka nimgawie mkeo maumivu yako, sikutaka akuumize tena na mimi nikiwepo. Nisamehe sana.β
Willy alishangaa, nilimtazama Willy na kusema βKaka unaweza kutuacha tafadhali.β
Willy alinitazama na kusema βbila shaka kaka.β
Aliinuka na kutoka zake.
Alipotoka nilipambana nikakaa, na yeye alinisaidia na kusema βHey my girl, napenda unavyonitetea, unavyo nipambania. Kusema kweli peke yangu bila wewe siwezi.
Umenipa nguvu ya kupambana, na kujiona nina thamani kubwa. Mimi najua uliyosema yote una maanisha Pina. Ina maana ulikuwa unatania kuwa unanipenda sana, utaniheshimu na kunijali sana.β
Pina alitabasamu na kisha alisema βRicky pleaseee!!β
Nilimvuta akae karibu yangu na nilimkumbatia na kusema βPleaseeeee!!, Pleaseeeeee!!, nakupenda.β
Akaniambia kwa upole βWapo sahihi, sikustahili, siendani na wewe, sivutii, sioni, maskini na bado ninaye mtoto, zaidi ya hayo yote nina maumivu makali.β
Nilisema kwa upole βPina mimi ndiyo sikustahili, siendani na wewe, sivutii, sioni na mimi ndiyo maskini kwasababu ni
Mjinga na mpumbavu niliacha mjinga kama yule atawale hisia zangu.β