
LOML | Love Of My Life (172)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:172
Nilimtazama Willy na kusema “Moyo umechoka sana, Nipo hapa kwasababu ya mambo yake ya ajabu. Willy kwa alicho nifanyia hata mbinguni sidhani kama bado tupo kwa orodha ya wanandoa. Ndoa yetu imekufa kabisa.
Nikitoka hapa, kabla ya kwenda popote ni kanisani kufuatilia taraka. Tena natamani iwe haraka sana na nifanikiwe kwenye hili. Kusema ukweli sitamani hata kukumbuka mimi ni mume wake au nimewahi muoa. Ni mshenzi sana.”
Willy alishangaa na kuuliza “ni serious namna hiyo?”
Nilisema kwa upole “nashangaa hata ujasiri huo ametoa wapi kuonekana na kujiliza kwangu. Alipaswa kuona aibu, na kujificha maisha yote. Kaka ipo siku nitakuelezea haya kwasasa acha nipumzike tu sitaki kuteseka lakini niambie vipi Pina?”
Willy alitabasamu na kusema “Nimempenda.”
Nilimtazama na kusema “ongea vizuri kaka, umempenda aje sasa shemeji yako yule.”
Willy alicheka akisema “umekamatika kaka, toto zuri lile aiseee, halafu haachi kunishangaza. Mmenipa raha sana.”
Nilitabasamu nikisema “nitumie ile video.”
Akacheka akisema “nilijua tu lazima, lazimaaa!!”
Tulicheka, na mwisho wa yote alinitumia video, akaniaga na kuondoka zake nilibaki chumbani peke yangu. Nilikuwa namuwaza tu Pina wangu, na kutabasamu hata nikapitiwa na usingizi.
Ulipita muda kidogo tu, baba yangu aliingia na aliniamsha. Nilipoamka baba yangu alinikumbatia kwa furaha sana na kusema “mwanangu una shida gani, unapata tatizo husemi mpaka unalazwa umenyamaza tu, au unatuchukia wazazi wako maana sijakuelewa. Hata mimi msiri wako, eenh kijana wangu. Unajua wazi mimi bila wewe sio kitu. Wewe ndiyo nguvu yangu na sasa unataka nife au wewe ufe nilie mpaka udongo unimeze na mimi.”

