
LOML | Love Of My Life (174)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:174
Nililia nikisema βbaba yangu, nawezaje kujizuia, sikutaka kumuoa yeye mimi na hapo sikuwa hata na mtu niliyewahi kumpenda. Niliwatii ninyi wote nikamuoa na kumpa zawadi ya upendo ambao hastahili. Lakini amefanya nini, baba amefanya nini hafai. Sitaki kusikia jina lake, sitaki kumuona tena kwenye maisha yangu. Amekufa kwangu, sio mke wangu tena na sitamani kumuona.Nikitoka hapa baba ni taraka, siwezi kuishi na shetani.β
Baba alinikumbatia kwa upendo, na aliniambia kwa upole βniambie mwanangu, niambie baba yaki nipo hapa, nipo hapa baba yako.β
Unajua ukiwa na maumivu halafu upo na mtu anakuelewa, siku hii niliamua kufunguka ukweli wa mke wangu kwa mara ya kwanza kwa baba yangu mzazi kuanzia alivyo anza kunihamishia sehemu, baba alikuwa anatikisa kichwa anasema βtobaaa!!, tobaaa!!!, si laana hii.β
Yaani angejua la mbele hata angekutunza masikitiko yake kwanza maana atazimia kabisa. Nikaendelea wanaume wale akiwepo Max, mc na Dokta.
Baba alizidi kusikitika sana, na hata nikawa nasema natamani nikuoneshe na ushahidi baba ila haiwezekani wewe ni baba yangu, lakini nayo yote nilisamehe na kuwatii wazazi wangu. Niliongea na mama yake nikaamini na nikawa tayari kumbeba na kumsaidia mke wangu.
Lakini baba kumbe hayo yote ni kivuli, mke wangu ni msagaji, msagaji baba.β Hapa nilijikuta nalia kwa nguvu, hata baba alinitazama kama anataka kulia na kuniuliza βmsagaji?, ni nini maana yake, sijaelewa kijana wangu. Anasaga unga?, hupendi akisaga unga maana hapo ndiyo kusaga na kukoboa mimi sikuelewi, acha kuzunguka ana saga nini mwanangu?β
Nilimtazama na kusema βmke wangu baba, mke wangu ana fanya mapenzi ya jinsia moja, kwa macho yangu nimemkuta anafanya mapenzi na mwanamke mwenzake kitandani kwangu kwa macho yangu baba.β