
LOML | Love Of My Life (177)


𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:177
Baba alikuwa anatabasamu na kunong’ona akisema “ni mrembo sanaaa unajua kuchagua mwanangu una jicho.”
Hata nilitaka kucheka na Pina alisema “Nisamehe sana Ricky, sikujua una mgeni.”
Nilitabasamu na kusema “karibu Pina, ni baba yangu. Anatamani kukusalimia.”
Pina alitabasamu, kisha alichuchumaa kidogo akisema “shikamoo baba!!”
Baba alinitazama kisha alisema “marahaba binti yangu, haujambo.”
Pina alijibu salamu kwa tabasamu , na baba aliendelea “karibu uketi mwanangu karibu.”
Pina akawa anapiga hatua na fimbo yake, baba yangu kwa upendo alimsaidia. Pina alitabasamu na kusema “nashukuru sana baba, nashukuru kwa upendo.”
Baba alimtazama Pina ni kama alikuwa anamuhurumia hivi na kusema “karibu mwanangu, ina maana huoni, macho yako ni kama yanaona.”
Pina alitabasamu na kusema “upo sahihi baba lakini ni kweli sioni.”
Baba alinitazama na kusema “sijui kwanini, ila naona ana uwezekano mkubwa wa kuona namna ninavyo muona ni kama anaona kabisa. Kwani umezaliwa hivi mwanangu.”
Pina alitabasamu na mimi nikawa natabasamu tu, baba yangu ana huruma sana unajua hata alisema “hapana baba, mitihani tu.”
Baba aliongeza “umewahu kwenda hospitali?”
Pina alisema kwa upole “sahihi baba, niliwahi gharama za matibabu ni kubwa sana.”
Baba alisema “hapana hutakiwa kuwa hivi kama Mungu hakupenda uwe hivi binti yangu. Najua gharama ni mtihani ila kama utakubali mimi nitakusaidia utapona, si upo tayari.”
Pina alitabasamu na kusema “unasema kweli baba?”