LOML | Love Of My Life (178)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:178
Baba alitabasamu ba kusema β€œnimetokea kukuhurumia sana, na kwasababu kijana wangu anakupenda nami nakuona kama binti yangu. Nitapambana upone. Endeleeni mimi natoka nitarudi.”

Baba yangy alionekana kampenda sana Pina. Umewahi kwenda mahali tu unapendwa mpaka unashangaa ndiyo Pina sasa. Alifurahi akanikumbatia akisema β€œbaba yako ni mzuri sana, ana maanisha nitapona kweli?”

Nilitabasamu na kusema β€œbaba huwa hatanii hapo usikute kaenda zake kitengo cha macho.”
Pina alisema β€œmiaka minne hiyo ilikuwa Milion 7 kunitibia sasa si itakuwa gharama sana.”

Nilitamani kucheka maana kwa baba hiyo hata sio pesa. Nilimwambia β€œmuamini tu, utaona hata iwe 20 baba akikuahidi lazima atimize.”

Alinitazama na kusema β€œuna bahati sana, kuwa na baba kama huyu niamini, ila mke sasa mkali kama nini?”

Tukacheka, Pina aliendelea kusema β€œsasa natamani sana kukuona, natamani kuona namna ulivyo mzuri wa moyo na uso wako, natamani kumuona kijana wangu akikua, na sasa baba yako malaika wangu mwingine ambaye anataka kuja kukusaidia, na bado ninaye bibi.

Mungu sikia maombi yangu, maombi yangu ni kuona naona Mungu ananijibu kwa namna ambayo sikudhani kabisa.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

CHAGUO LA MOYO FULL

TOBO LA PANYA FULL

UTAMU WA JAMILA FULL