
LOML | Love Of My Life (179)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:179
Nilimtazama na kutabasamu nikisema “wewe ndiyo maombi yangu ambayo nilimuomba Mungu. Pina mimi nakupenda sana na nitafanya lolote ujue kuwa nakupenda sana. Ninakupenda mno.”
Pina alitabasamu na kusema “chakula, kinapoa sasa. Tule kwanza.”
Nilitabasamu na kusema “ unataka kuniambia ulienda nyumbani kupika?”
Alitabasamu na kusema “nilisikia muda ule mke wa Willy ndiyo kapika nikaona sio mbaya nimsaidie.”
Nilimtazama na kusema “ungesema basi nikupe pesa ukanunue chakula.”
Alinitazama na kusema “kumbe hospitali wanagawa pesa kwa wagonjwa mbona sijui nianze kuumwa pia.”
Nilicheka sana nikisema “unajua wewe huna akili?”
Alicheka na kusema “upo sahihi, lakini wewe huna kabisa haya sasa nisaidie niweke vizuri nisimwage.”
Nilipokea mfuko na kumsaidia kupakua chakula na kuweka kwa sahani. Zilikuwa sahani za plastiki ila nilifurahia sana. Ndizi hizi na utumbo vimeandaliwa kwa upendo sana.
Nilikuwa nahamu ya kula kweli. Tulisali, na kisha alinilisha kijiko kimoja nikasema “ni bibi sio wewe, huwezi kupika ndizi tamu hivi.”
Alicheka na kusema “unafanya masihara ernh, mimi najua kupika sana acha masihara. Bibi yangu anajua lakinj unajua vya kurithi vinazidi.”
Nilisema nikitabasamu “acha kuongea naomba chakula.”
Alitabasamu akisema “umekipenda eemh, naona umekipenda sana.”
Nilitafuna nikisema “sanaaaa, unajua naona kama nimepona hivi?”

