
LOML | Love Of My Life (18)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:18
Ndoa sio tu kuhusu kupenda au kutokupenda. Wakati mwingine ukikosa kabisa cha kufanya kupenda ndiyo chaguo. Ndoa ni Mungu peke yake kaka. Ninayo imani utafurahia ndoa yako. Sio ndoa zote zina furaha kuna wakati mambo hayaendi kabisa ndugu yangu.
Wewe shikilia kamba, mwisho wa siku mtakuwa sawa na mtapendana sana. Niamini mimi, naona kabisa utaweza ndugu yangu. Sio tu unaanza kufuata kile unahisi moyoni, kaka niambie ukweli au una mwanamke una mpenda?β
Nilimtazama na kutabasamu, kusema ukweli ninampenda sana yule mwanamke, nina mpenda sana lakini sasa sijafikia kukiri hivyo kuwa nampenda maana hata sina hakika kama nitamuona tena au hapana. Nilimtazama kaka yangu huyu na kusema βhapana kaka, hakuna kitu kama hicho. Kuna muda nafikiri ni woga tu na kujiona sipo tayari kwa ndoa lakini utaisha na nitafurahia ndoa yangu na mke wangu.Kwasababu ni mwanamke mzuri sana.β
Tulijikuta tunacheka na kuanza kutambiana nani mzuri sana na vitu kama hivu si unajua tena utani wa wanaume. Tuliongea mengi sana. Ila kubwa zaidi tulizungumza kuhusu ndoa yangu kuipa nafasi na kusema ukweli kutoka moyoni mwangu nilikuwa tayari kuanza kupambana, kumpenda mke wangu maana ndiyo tayari kawa mke wangu hakuna namna nyingine. Nilikuwa nafurahia vile Willy ananipa kila sababu za kumpenda mke wangu.
Wakati huo mke wake sasa, kuna wanaume wamepata wanawake wazuri sana. Mwanamke ana andaa chakula kwa upendo sana, kaandaa kwa upendo, hata nilikuwa nashangaa mimi. Vile amekuja pale tumeketi na kusogea karibu na mume wake.
Anaongea kwa heshima, amesimama kwa heshima halafu sasa alivyo valia kwa heshima, mpaka mimi mgeni nasema βhivi ndiyo yupo hivi au ananigizia hapa.β
Vile anazungumza βmume wangu, karibu kula, chakula kipo tayari mume wangu.β