LOML | Love Of My Life (180)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:180
Tukacheka, nakumbuka nilimshika uso wake na kusema β€œukiwa na furaha kama hivu una kuwa mzuri zaidi, unanivutia zaidi mpenzi wangu. Pina kama kuna mtu hajawahi kukuambia ulivyo mzuri. Sidhani kama amekutana na watu wazuri duniani.

Binafsi sina mfano wa kutosha kuelezea namna ulivyo mzuri. Wewe ni mzuri sana, ni kazuri mno. Unanichanganya, nakupenda sana.”

Pina alitabasamu na kuniambia akinipapasapapasa usoni, β€œhisia zangu hazidanganyi, sijawahi kukutana na mwanaume mzuri kwenye hii dunia kukushinda wewe. Sina macho lakini nakufahamu tayari. Wewe ni bonge la handsome na macho yako makubwa hayo nakupenda.”

Nilicheka na kusema β€œumejuaje nina macho eneh, umejuaje,”
Alitabasamu na kushika, na kusema β€œkwa kugusa, kushika, kuhisi najua vitu vingi. Wewe ni mwanaume mwenye mvuto Ricky, una macho mazuri yaliyo jaa huruma na upendo. Haya kula sasa..”

Nilitabasamu na kusema β€œsasa mbona hujamalizia My smiley!!!”
Alitabasamu na kusema β€œMy fortune.”
Nilitabasamu na kusema β€œMy fate.”

Kisha nikawa namtazama vile anatabasamu, nikachukua kijiko na kumlisha pia, alinishukuru na nikawa naendelea kulishwa huku nikimuelezea nimeongea na baba kuhusu Gabby na namna amepokea. Pina alisema kwa upole β€œpole sana Ricky, haujachelewa bado na sitaki kuingilia sana suala hili. Lakini nipo hapa na wewe ukinihitaji nipo hapa.”

Nilitabasamu na kusema β€œnajua ni ngumu kunielewa, lakini umenipa sababu ya kuwepo, sababu ya kupumua kwa nguvu zangu zote na kupambania maisha yangu. Nakupenda.”

Nilimshika mashavu na kumbusu, nikawa namtazama na wakati huo Willy na mke wake wanaingia, na nikatabasamu nikisema β€œkaribu sana shemeji.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

KIBOKO YANGU FULL

CHAGUO LA MOYO FULL