
LOML | Love Of My Life (181)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:181
Shemeji yangu alitabasamu na kusema “pole sana shemeji yangu.”
Willy alicheka na kusema “shemeji yako hapo roho kwatu alijua sijui nashinda wapi usiku kapambana aje haya sasa mgonjwa huyu hapa.”
Tulicheka tu, kisha nilimtambulisha Pina, mke wa Willy hanaga maneno yeye ni heshima tu. Tulikuwa tunacheka pale hata baba aliingia. Walimsalimia na kisha alisema “Mwanangu, unaweza kunifuata mara moja?”
Tulitazamana, kisha baba alisema “Pina binti yangu unaweza kunifuata?”
Nilitabasamu na kusema “nilikuambia mimi, sasa si umeona.”
Pina aliinuka, baba yangy alimshika mkono na huku Willy akiniuliza “wanaenda wapi tena?”
Nilitabasamu na kusema “wapi kama sio kwa dokta wa macho. Si unamjua baba Ricky?”
Willy alisema “wee usinambie, mzee wako ana upendo sana lakini na hapo tena roho ya kijana wake. Maskini Pina haamini pale.”
Nilitabasamu tu, huku shemeji akisema “nafurahi kuona unaendelea vizuri shemeji yangu.”
Nilitabasamu na kusema “nashukuru kwa upendo na chakula. Ubarikiwe sana.”
Alitabasamu tu, na kisha alisema “na leo nimebeba ila nishawahiwa.”
Tukacheka huku Willy akisema “tutakula wenyewe kwanza mimi mwenyewe nina njaa.”
Mke wake alisema “baba huna aibu wewe cha mgonjwa ujue.”
Basi tulicheka sana.
Muda ulizidi kwenda baba na Pina hawakurudi hata Willy na mke wake waliaga na nikabaki peke yangu. Baada ya muda walirudi, Pina hakuonekana kuwa na furaha. Nikauliza “baba kuna nini tena?”
Baba aliniambia “usijali mwanangu, dokta wamemchek, kadri anavyozidi kukaa na hali hii bila kutibiwa anazidi kuharibikiwa. Lakini wameshauri twende India. Na nimeona ni kitu kizuri.

