
LOML | Love Of My Life (182)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:182
Na naahidi tena kuwa utakapo maliza mambo yako, wewe na yeye mtaenda huko na ataona tena bila kujali daktari wanasema nini. Ondoa hofu binti yangu hakuna gumu chini ya jua.
Wakati mwenzako anashughulika na mambo yake mimi nitawatafutia utaratibu mzuri na nitaweka sawa kila kitu mtaenda huko.β
Pina alimkunbatia baba kwa nguvu, alilia akisema βnashukuru sana baba, Mungu akubariki sana.β
Baba alikuwa hawezi hata kusema kitu, alikuja na kunikumbatia kwa nguvu, nilifurahi sana. Baba alinitazama na kusema βnatoka wanangu, tutawasiliana sawa.β
Nilisema kwa upole βbaba yangu kipenzi, nashukuru kwa kila kitu. Wewe ni baba bora sana kwangu.β
Baba alitabasamu na kusema βnakupenda sana mwanangu. Napenda furaha yako.β
Nilitabasamu, na baba aliendelea βanything for you my boy!!β
Nilitabasamu na kusema βgat you dady!!β
Alitabasamu na kutoka akisema βPina mlinde huyo narudi tena.β
Pina alitabasamu na kisha alianza kulia akisema βnamshukuru sana Mungu kwa kunikutanisha na wewe. Kila kitu kinazo sababu, na kumbe ili mimi kupona ilikuwa ni lazima niwe na wewe. Ricky, nashindwa kujizuia, nashindwa kabisa. Baba yako, hakuna mtu amewahi nitendea kama yeye au wewe. Ninyi ni watu wa sayari gani.β
Nilitabasamu nikisema βPina tulia kwanza sawa mumy, mambo madogo nakuahidi kesho tunatoka hapa ili nikaanze kushughulikia haya na kisha utaona lazima.β
Pina alilia akisema βnaikumbuka sana ile siku Ricky, naikumbuka nilimuacha mwanangu, na kwenda kupika. Huku napika na mshono wangu wenye maumivu, mtoto analia na mimi nahangaika na jiko.Nilipika, nilipika mpaka nikamaliza.