LOML | Love Of My Life (183)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:183
Na baada ya hapo ndiyo nilikula. Huwezi kuamini, baada ya kurudi wao kwenye mambi yao walikula tena bila hata hofu yoyote chakula nilichopika hata pole sikupewa. Nilijisikia vibaya sana na ndani yangu niliona kabisa sitaweza kukaa pale. Niliona kabisa bora niondoke nirudi kwangu.

Usiku wa siku hii hali yangu na hasira ndiyo usiseme. Unajua vile unakaa mahali halafu unajua kabisa hawakutaki ndiyo mimi sasa. Kesho yake tulipoamka tena mzazi mwenzake na mume wangu alikuja.

Mama anamwambia β€œingia kamuone mwenzako, mtoto sijui hata kafanana na nani kati ya mama na baba yake. Ingia tu hakuna shida.”
Mimi nawasikia, sijakaa hata vizuri akaingia chumbani kwangu na kusema β€œmnaendeleaje?”

Nilimtazama tu na kushindwa hata kujibu, akawa anamtazama mtoto halafu anasema β€œmama, huyu mama yake kwa baba yake hayupo hata unajua hayupo.”
Mama mkwe anasema β€œmimi naona kama baba yake eti, au sioni vizuri.”
Nilimchukua mtoto wangu na kumpa nyonyo maana nilikuwa naona wananichosha tu.

Alitoka chumbani, nilijiambia moyoni β€œMungu nipe uvumilivu, nipe Uvumilivu Mungu wangu.”
Basi nilikuwa tu nakaa chumbani na mtoto wangu na asubuhi ilikuwa ni siku ya kwenda kusafisha kidonda changu. Niliamka nikajiandaa, nikamfuata mama na kumuomba twende hospitali.

Mama alikataa na kusema β€œkwani una shindwa nini kwenda mwenyewe mbona wazazi wa sikuhizi mnadeka sana.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata