LOML | Love Of My Life (186)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:186
Ninakumbuka siku iliyofuata, ilinibidi niamke, macho yanauma, sioni hata mbele vizuri. Nilijiandaa mpaka kwa mama mkwe wangu. Aliponiona tu alisema β€œmalkia ndiyo anafika.”

Nilijia tu ni kejeli, nilisalimia na alinijibu akiendelea kuchezea simu. Nikamuulizia juu ya mume wangu. Akanitazama na kusema β€œem kamuangalie huko chumbani.”
Nilishusha pumzi, wakati naenda akaniambia β€œniletee mjukuu wangu mie.”

Akitaja jina la mtoto la kikwao ambalo yeye ndiyo alitoa. Niliingia kwenye kile chumba, nilikuta mume wangu amelala na mzazi mwenzake nyumbani kwao. Nilichoka. Mbaya zaidi mume wangu hajali hata hashtuki halafu huyo mzazi mwenzangu anacheka sana.

Nilitoka nalia na kumchukua mtoto wangu bila hata kutia neno huku mama mkwe akicheka sana. Walikuwa na mahusiano, sijui sana kuhusu mahusiano yao ila namna ilivyo naona ni zaidi maana msichana anapendwa na kujiamini sana.Nilipofika nyumbani nililia sana, nililia kupita kiasi familia hainipendi na mume wangu pia hanipendi na ndiyo kwanza nimejifungua.

Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa maumivu, mume wangu hakutuma text wala hakuniuliza kitu alinyamaza. Nilikuwa naendelea kumtafuta wakati najua ana mahusiano mengine. Macho nayo yalizidi kunitesa. Ilinibidi niende hospitali. Nikapewa tu dawa ya macho na nilipoanza kutumia ndiyo mambo yalipozidi kuwa mabaya kwangu. Macho yaliuma sana, nakumbuka nyakati zote hizi nilikuwa peke yangu, mume wangu anarudi na kuondoka hanipi hata nafasi ya kuzungumza. Anatuma pesa.

Mtoto wangu alianza kuumwa, nikawa najipa moyo atajisaidia kesho kesho inapita hivyo hivyo hajisaidii. Siku zilizidi kusogea. Mtoto wangu alikuwa hapati choo. Macho yangu nayo yalizidi kupamba moto.

Nilienda hospitali, hospitali walinipa dawa lakini unajua mtoto asipopata choo anavyolia na kuhangaika. Nilimtafuta baba yake ambaye alikuwa kwao na mzazi mwenzake kumuelezea hili lakini wapi. Hakuna aliyejali.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

KIBOKO YANGU FULL