LOML | Love Of My Life (191)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:191
Nilichukua usafiri na kurudi mpaka kwangu. Hapa nilipofika nilikuwa nalia tu nilikuta mwanangu bado anajisaidia. Hivyo hivyo nikabeba nguo zetu na kumwambia bibi yangu kuwa tunaenda kwake.Bibi alishangaa na kuniuliza β€œkuna nini?”

Nilimuuliza bibi β€œunataka waniue bibi, Hakuna mtu ananihitaji tuondoke. Watatumaliza.”

Bibi yangu anasali sana, alinichukua hapa tukachukua usafiri ndiyo kurudi kwa bibi yangu. Nilichoka sana. Saa 6 mtoto ndiyo alimaliza choo. Kwakuwa nilichoka nikalala.

Bibi alikuwa na mtoto wangu. Mida ya saa 9 nilihisi mkojo, niliamka, nilipoamka kwa macho yangu mawili nilimuona mama mkwe na mtoto wake, wakiwa wanacheza chumbani kwangu, mama mkwe kavalia kitenge kifuani na mume wangu kavalia kikoi kiunoni. Nilishangaa na kuita β€œmume wangu!!!”

Walishtuka, nikaita tena β€œmama!!, Kumbe nyie ni wachawi?, mnataka nini kwangu kuniua au kitu gani?”
Mume wangu alinipulizia unga, palepale nilipiga kelele β€œbibiiii wamekuja, wachawiiii, bibi sioniiiii, sioniiiii!!!”

Bibi alikuja mbio chumbani, nikawa nalia tu. Na akatoka kuomba msaada. Nikapelekwa hospitali. Hapakuwa na maendeleo nikaamishiwa CCBRT nikiwa sioni chochote. Baada ya vipimo nilionekana kama nimetumia şumu ambayo taratibu ilikuwa Ina affect macho yangu na kwamba nitakuwa kipofu.

Nililia nikiuliza kama naweza tibika, walisema inawezekana Ila kwa wakati huo hatukuwa na pesa. Sitaki kukumbuka hii siku, kuanza maisha mapya, kutembelea fimbo na kuishi kwa hisia.

Ninajua kilichotokea, lakini majibu yanaonesha nilikuwa na sumu. Sasa nawaza au ile dawa ya mama mkwe?, sio kila kitu cha kupokea tu ili mradi unaambiwa dawa Kumbe wengine wanakupa sumu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata