LOML | Love Of My Life (192)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:192
Bibi yangu ndiyo alikuwa msaada kuanzia pale, maumivu, mateso ya kuomba omba, kunyanyasika, kukubali hali mpya kutoka kwa mwanaume niliyempenda haikuwa rahisi lakini kilinifanya niwe karibu sana na Mungu.

Tangu hapo sijawahi hata kujua maisha Yao, wala kusikia habari zao. Naamini Mungu amewapa wanacho stahili. Yapo Mengi Ila nimeamua kufupisha walau ujue nilivyoishi kwa mateso.

Kuna muda nasali sijui nitapata muujiza au natakiwa kupona hospitali. Δ°mani yangu inaniambia nitapona lakini sielewi, mwanangu Nilimtazama naishia kusema asante Mungu. β€œ

Nilimuhurumia nikisema β€œinatosha Pina, inatosha unajua tunatakiwa kufurahi. Tuunganishe haya maumivu tuwe kitu kimoja. Stop weeping, Nakupenda sana. Sahau hayo yote ulikuwa lazΔ±ma upite ili umjue Mungu namna hii. Nakuomba usilie.”

Pina alinikumbatia na mimi nilimkumbatia. Ulikuwa usiku mzuri sana, hata baba yangu hakurudi hapa. Na asubuhi nilipoamka, Pina alikuwa amenishika mkono anasali, alipomaliza nilisema β€œAmen.”

Alitabasamu na kusema β€œNaona leo umeamka vizuri. Good morning handsome wangu, Mimi naomba nikuache Mara moja nitarudi Baada ya muda nikamsaidie bibi kazi.”

Nilimwambia kWa upole β€œSubiri nikuitie dereva.”
Aliniambia kWa upole β€œHapana mpenzi usimsumbue nitafika.”

Nilikataa na kusema β€œHaiwezekani.”
Nilichukua simu na kumpigia Dereva, kweli Baada ya muda alimfuata na mimi nilikuwa hapa. Siku hii niliamka vizuri, hata nilimuomba dokta nitoke.

Nakumbuka niliambiwa nisubiri nikawa tu nakumbuka hadithi ya Pina najisikia vibaya wakati kuna wanawake wajinga Kumbe na wanaume pia ni wengi. Baba alinipigia, akaniuliza Hali yangu nikamuelezea Nimeomba kutoka.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata