
LOML | Love Of My Life (198)

πππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:198
Ninatamani nikuambie kitu kuhusu kitanda unacho lalia. Kama kimebeba roho za watu wengi mpaka unapata mpenzi wa maana bado unalalia hikohiko na huyo mpenzi wako au mume wako naomba sana jitahidi ukibadilishe.
Mapenzi ndiyo kitu pekee kinaunganisha roho zetu na kuhamisha vitu kutoka nafsi moja kwenda nyingine. Na sio kila mtu ambaye unalala naye ana roho nzuri.
Wengine wana roho mbaya sana, wamebeba vitu wanavyojua ai wasivyojua, laana za ukoo na mambo ya dunia na unapolala naye tu anakugawia na wewe na kukuachia hapo kitandani kwako na basi ndiyo maana unatakiwa uombee sana kitanda chako maana nacho kinahusika sana kwa asimilia kubwa sana kubeba baraka za maisha yako.
Kama mahusiano au ndoa ina kusumbua haujui tatizo na kitanda chako unajua kimepitia mahusiano ya kutosha jaribu kukibadilisha na uanze kutamkia mema hiko kitanda kingine utaona mabadiliko makubwa kwa maisha yako. Chumba chako, kitanda chako ni sehemu kubwa ya maisha yako ya mafanikio.
Nadhani unakumbuka hadithi ya Pina alikuwa anajua amepata mume kumbe ni mchawi na mama yake kwake walikuwa na yao tu. Wewe unalala naye na humjui kwa undani.Binadamu ndiyo tulivyo ni wazuri wa kutazamana lakini roho zetu ni zinatisha sana.
Nilisogelea mahali Pina alikuwa amekaa, nilimtazama alikuwa ametulia. Nilichuchumaa mbele yake nikisema βasante kwa kuja Love of my Life.β
Alitabasamu na kusema βnimefurahi kuwepo hapa. Hongera ni pazuri sana.β
Alikuwa kama mtu ambaye ana tazama huku na kule. Hata nilikuwa ninamtazama tu na nilisema βSio pazuri kama ulivyo mzuri wewe Pina wangu.β
Alitabasamu, na nikaona kama mtu ambaye anatokwa na machozi. Nilimfuta na kumuuliza βhujafurahi kuwepo hapa?, kwanini unalia mama angu.β
Alinishika uso wangu na kusema βnatamani ningepata kuona hata kwa sekunde tu, moyo wangu unatamani kukuona, unatamani kujua ni nani amefanya nijisikie hii amani.
Ricky, ni ngumu kunielewa lakini namna ninajisikia kuwa karibu na wewe sijawahi kujisikia hivi kabla. Ni ajabu, ni ajabu kubwa sana. Ninaona ninakupenda na siwezi kujizuia kabisa.

